Malkia ni kete ya mchezo wa sataranji ambayo inasimama karibu na shaha mwanzoni mwa mchezo.
Malkia hukaa kwenye mraba d1 kwa upande mweupe na mraba d8 kwa upande mweusi. Inaweza kusogea idadi yoyote ya miraba isiyokaliwa kwa mshazari, wima, au mlalo . Wakati wa kurekodi michezo, inatajwa kwa kifupi cha "Q".
Malkia hutazamiwa kuwa kete yenye uwezo mkubwa kushinda zote kwenye sataranji.
Malkia anaweza kusogea kama sataranja (bishop) na ngome (rook). Kila mchezaji huanza na malkia mmoja. Mchezaji anaweza kubadilisha kitunda kuwa malkia wakati kinafika mstari wa mwisho wa ubao.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Malkia (sataranji), which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.