Majimbo Ya Afrika Kusini

Majimbo ya Afrika Kusini ni ngazi ya kwanza ya ugatuzi nchini Afrika Kusini.

Nchi imegawanywa katika majimbo tisa. Katika mkesha wa uchaguzi mkuu wa 1994 nchi ilikuwa na majimbo manne halafu kulikuwa na maeneo ya bantustan. Kabla ya uchaguzi huo wa kwanza ulioendeshwa bila ubaguzi wa rangi maeneo ya bantustan yaliunganishwa tena kisheria na Afrika Kusini na nchi yote iligawiwa kwa majimbo tisa.

Majimbo Ya Afrika Kusini
Majimbo ya Afrika Kusini

Historia

Majimbo Ya Afrika Kusini 
Majimbo manne wakati wa kuunda Muungano wa Afrika Kusini mnamo mwaka 1910

Muungano wa Afrika Kusini ulianzishwa mwaka 1910 kwa kukuunganisha makoloni manne ya Uingereza: Koloni la Rasi, Koloni ya Natal, Koloni ya Transvaal na Koloni ya Mto Orange (hizi mbili za mwisho zilikuwa hadi uvamizi wa Uingereza jamhuri huru za Makaburu zilizojulikana). Makoloni haya yakawa majimbo manne asilia ya Muungano: Mkoa wa Cape, Mkoa wa Transvaal, Mkoa wa Natal na Dola Huru la Oranje .

Majimbo Ya Afrika Kusini 
Majimbo na maeneo ya bantustan kama ilivyokuwa mwisho wa ubaguzi wa rangi

Wakazi wasio Wazungu walibanwa katika maeneo maalum kuanzia mwaka 1913. Umiliki wa ardhi kwa watu weusi ulizuiliwa kwa maeneo fulani ya jumla ya 13% ya nchi yote. Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1950, maeneo haya yalibadilishwa hatua kwa hatua kuwa "homelands" au "bantustan". Nne kati ya nchi hizi zilitangazwa kama nchi za pekee za watu weusi wakati wa enzi ya apartheid . Mnamo 1976, nchi ya Transkei ilikuwa ya kwanza kukubali uhuru kutoka kwa Afrika Kusini, na ingawa uhuru huu haukuwahi kutambuliwa na nchi nyingine yoyote, nchi zingine tatu. – Bophuthatswana (1977), Venda (1979) na Ciskei (1981) – zilifuata kukubali uhuru bandia.

Tarehe 27 Aprili 1994, tarehe ya uchaguzi wa kwanza usio wa ubaguzi wa rangi ambako pia Katiba ya Muda ilipitishwa, majimbo haya yote na nchi za bantustan zilivunjwa, na majimbo tisa mapya yalianzishwa.

Orodha

Jimbo Jina kwa lugha inayotumiwa zaidi jimboni Mji mkuu Mji mkubwa Eneo: 9  Wakazi

(2022)
Densiti

(2022)
Ramani
Eastern Cape iMpuma-Koloni (Kixhosa) Bhisho (Bisho) Gqeberha (Port Elizabeth) km2 168 966
(sq mi 65 238)
6,676,691 /km239.5
(/sq mi102)
Majimbo Ya Afrika Kusini 
Free State Freistata (Kisotho) Bloemfontein Bloemfontein km2 129 825
(sq mi 50 126)
2,921,611 /km222.5
(/sq mi58)
Majimbo Ya Afrika Kusini 
Gauteng eGoli (Kizulu) Johannesburg Johannesburg km2 18 178
(sq mi 7 019)
16,098,571 /km2885.7
(/sq mi2 294)
Majimbo Ya Afrika Kusini 
KwaZulu-Natal iKwaZulu-Natali (Kizulu) Pietermaritzburg Durban km2 94 361
(sq mi 36 433)
11,538,325 /km2122.3
(/sq mi317)
Majimbo Ya Afrika Kusini 
Limpopo Limpopo (Kisotho) Polokwane (Pietersburg) Polokwane km2 125 754
(sq mi 48 554)
5,941,439 /km247.2
(/sq mi122)
Majimbo Ya Afrika Kusini 
Mpumalanga iMpumalanga (Kiswazi) Mbombela (Nelspruit) Mbombela km2 76 495
(sq mi 29 535)
4,720,497 /km261.7
(/sq mi160)
Majimbo Ya Afrika Kusini 
North West Bokone Bophirima (Kitswana) Mahikeng (Mafikeng) Rustenburg km2 104 882
(sq mi 40 495)
4,186,984 /km239.9
(/sq mi103)
Majimbo Ya Afrika Kusini 
Northern Cape Noord-Kaap (Kiafrikaans) Kimberley Kimberley km2 372 889
(sq mi 143 973)
1,308,734 /km23.5
(/sq mi9.1)
Majimbo Ya Afrika Kusini 
Western Cape Wes-Kaap (Kiafrikaans) Cape Town Cape Town km2 129 462
(sq mi 49 986)
7,212,142 /km255.7
(/sq mi144)
Majimbo Ya Afrika Kusini 
Republic of South Africa iRiphabhuliki yaseNingizimu Afrika (Kizulu) Pretoria,

Bloemfontein

Cape Town
Johannesburg km2 1 220 813
(sq mi 471 359)
60,604,992 /km249.6
(/sq mi128)
Majimbo Ya Afrika Kusini 

Tanbihi


Tags:

Afrika KusiniBantustan

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Mkoa wa IringaRushwaOrodha ya majimbo ya MarekaniWilaya ya NyamaganaSimba S.C.KengeMkoa wa KageraWanyama wa nyumbaniPaka-kayaMaliMashuke (kundinyota)MkonoSayariUenezi wa KiswahiliMselaBarabara nchini TanzaniaMoscowAli Hassan MwinyiMafumbo (semi)Ligi Kuu Tanzania BaraChawaOrodha ya Makamu wa Rais TanzaniaOrodha ya Marais wa ZanzibarNzigeHoma ya matumboAustraliaKaswendeMaeneo ya Kihistoria ya Kitaifa ya TanzaniaMrisho MpotoPius MsekwaNg'ombeKakakuonaAwilo LongombaAntibiotikiWapareAsili ya KiswahiliOrodha ya miji ya TanzaniaJakaya KikweteFacebookOrodha ya viwanja vya michezo TanzaniaMdalasiniMoses KulolaKifua kikuuUtafitiOsama bin LadenUislamu nchini TanzaniaAzimio la ArushaTaswira katika fasihiLughaMagonjwa ya kukuSilabiMaadiliUgonjwa wa kuharaNominoBendera ya ZanzibarMkoa wa ManyaraMarekaniBahashaSikioKilimoDolar ya MarekaniInsha ya wasifuSabatoNomino za wingiMaumivu ya kiunoKiraiKampuni ya Huduma za MeliKamusi elezoSemiWaluguruUtamaduniMsumbijiDiraMalariaWito🡆 More