Muungano Wa Afrika Kusini

Muungano wa Afrika Kusini lilikuwa jina la Afrika Kusini kuanzia 1910 hadi 1961.

Kwa lugha rasmi za nchi jina lilikuwa "Union of South Africa" (Ing.) na "Unie van Zuid-Afrika" (Afr.).

Muungano Wa Afrika Kusini
Bendera ya Muungano wa Afrika Kusini 1912 - 1928
Muungano Wa Afrika Kusini
Bendera ya Muungano wa Afrika Kusini na Jamhuri 1928 - 1994

Ilianzishwa kama muungano wa koloni 4 za Kiingereza zilizokuwa Koloni ya Rasi, Natal, Transvaal na Dola Huru la Oranje. Nchi mpya iliundwa kama dominion ya milki ya Uingereza na kupewa serikali yake pamoja na mamlaka ya kujiamulia katika siasa ya ndani na kuwa na jeshi la kitaifa.

Waafrika, chotara na wenye asili ya Asia hawakuwa na haki za kiraia kwenye ngazi ya muungano; jimbo la Rasi pekee ilikubali haki za kupiga kura kwa wakazi wote waliokuwa na kiwango fulani cha Mali wakilipa kodi za kutosha; hapa idadi ndogo ya Waafrika ilikuwa na haki za kiraia kamili kabla ya siasa ya apartheid iliyofuta haki hizi.

Ofisi kuu za dola zilizambazwa katika majimbo mbalimbali kwa sababu viongozi walishindwa kuelewana juu ya mji mkuu mmoja. Makao ya serikali ilikuwa mjini Pretoria (Transvaal), makao ya bunge mjini Cape Town (Jimbo la Rasi) na mahakama kuu katika Bloemfontein (Dola Huru la Orange). Muundo huu unaendelea hadi leo.

Siasa ya apartheid tangu 1948 ilisababisha hali gumu kati ya Uingereza, nchi mpya za Afrika na Maungano ya Afrika Kusini. Hapo bunge liliamua kujitenga kabisa na Uingereza na kutangaza jamhuri nje ya Jumuiya ya Madola.

Tarehe 31 Mei 1961 nchi ilitangaza uhuru wake kama Jamhuri ya Afrika Kusini.

Tags:

Afr.Afrika KusiniIng.

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

MusaP. FunkUlayaKiambishi tamatiKadi za mialikoMamelodi Sundowns F.C.Fatma KarumeWimboLahajaNimoniaWaluguruTabainiTabianchiJumuiya ya Afrika MasharikiFran BentleyMtakatifu MarkoHussein Ali MwinyiSalaKifua kikuuMkoa wa SimiyuWatutsiViwakilishi vya urejeshiMaudhuiOrodha ya wanamuziki wa AfrikaUfugaji wa kukuNominoElimuVitenzi vishirikishi vikamilifuUvimbe wa koromeo usababishwao na streptokokiKarafuuAlama ya uakifishajiDiamond PlatnumzVita vya KageraUenezi wa KiswahiliMlongeTasifidaUnyenyekevuMtoto wa jichoVivumishi vya idadiOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaMrisho MpotoViwakilishi vya idadiBungeFisiMauaji ya kimbari ya RwandaVivumishi vya kuoneshaUgonjwa wa uti wa mgongoSoko la watumwaKiambishiUrenoBiasharaMivighaTungoBara la AntaktikiOrodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifaMwarobainiAnwaniYordaniHistoria ya UislamuMmeaWitoMshororoTetekuwangaViwakilishi vya pekeeNamba tasaUmoja wa AfrikaGabriel RuhumbikaAl Ahly SCWamasaiMikoa ya TanzaniaUfahamuMatumizi ya LughaVivumishi vya -a unganifuRedioSikioNomino za wingiKombe la Mataifa ya Afrika🡆 More