Luciano wa Samosata (takriban 125 – baada ya 180) alikuwa mhutubu na mwandishi kutoka mji wa Samosata katika Syria wakati wa Dola la Roma.
Lugha yake ya asili pengine ilikuwa Kisirya lakini kazi zake zote zilizohifadhiwa zimeandikwa kabisa kwa Kigiriki cha Kale. Mtindo wa maandiko yake ulikuwa hasa tashtiti ambamo alikejeli ushirikina na desturi za kidini.
Luciano alikuwa na athari kubwa katika fasihi ya Magharibi. Kazi zilizochochewa na maandishi yake ni pamoja na Utopia ya Thomas More, kazi za François Rabelais, Timon of Athens ya William Shakespeare na Safari za Gulliver ya Jonathan Swift.
Zaidi ya kazi 80 zinazoaminiwa kuandikwa na Luciano zimehifadhiwa. Luciano alilenga hadhira ya Kigiriki iliyoelimika sana, ya tabaka la juu.
Lucian alikuwa mmoja wa waandishi wa kwanza wa riwaya katika ustaarabu wa magharibi. Hadithi ya Kweli ( Ἀληθῆ διηγήματα ) ilikuwa kazi ya masimulizi ya kubuni. Katika hadithi hii aliiga baadhi ya hadithi za ajabu zilizosimuliwa na Homer katika Odisei na pia habari zilizorekodiwa na mwanahistoria Thucydides . Alitarajia mandhari ya kisasa bunilizi ya kisayansi ikiwa ni pamoja na safari za kwenda mwezini na hadi Zuhura, uhai wa nje na vita kati ya sayari. Riwaya hiyo mara nyingi huchukuliwa kuwa kazi ya kwanza inayojulikana ya bunilizi ya kisayansi.
|translator-link=
ignored (help); Unknown parameter |translator-last=
ignored (help); volume II; volume III; volume IV.|translator-link=
ignored (help); Unknown parameter |translator-last=
ignored (help); Check date values in: |accessdate=
(help); volume II.|translator-last2=
ignored (help); Unknown parameter |translator-link=
ignored (help); Unknown parameter |translator-link2=
ignored (help); Unknown parameter |translator-last=
ignored (help); volume II; volume III; volume IV.This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Luciano wa Samosata, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.