Internet Archive ni shirika lisilotafuta faida linalojenga kumbukumbu ya kidijitali kwenye intaneti inayopatikana kwa kila mtu bila malipo.
Makao makuu ya shirika yapo San Francisco, Kalifornia (Marekani). Lilianzishwa mwaka 1996 na Brewster Kahle.
Internet Archive ilianzishwa 1996 kwa shabaha ya kutunza yaliyomo ya intaneti kwa kuhifadhi picha za tovuti nyingi. Kwa hiyo inawezekana kuangalia picha za tovuti ambazo zimeshabadilishwa tena mara kadhaa.
Tangu 1999 hifadhi nyingine zimeongezwa. Sasa kuna vitengo vya video, filamu, picha na vitabu.
Kitengo maalumu cha IA ni maktaba ya "Open Library". Vitabu visivyo tena na hakimiliki vinapigiwa picha kila ukurasa kwa njia ya scanner na kuwekwa kwenye intaneti katika fomati mbalimbali.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Internet Archive, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.