Jost Gippert (; amezaliwa tar.
12 Machi mwaka 1956 katika Winz-Niederwingen, sasa: Hattingen, Ujerumani) ni mwanaisimu mjerumani na mwanamaarifa wa Caucasus. Yeye ni profesa kwa isimu ya mlingo katika chuo kikuu "Johann-Wolfgang-Goethe", Frankfurt.
Mwaka wa 1972 alihitimu masomo ya sekondari katika "Leibniz-Gymnasium", katika mji wa Essen-Altenessen. Tangu 1972 mpaka 1977 alijifunza isimu wa mlingo, usayansi wa India, usayansi wa Japan na usayansi wa China katika chuo kikuu Marburg na chuo kikuu huru Berlin. Baada ya masomo aliupata udaktari wa Falsafa (Ph.D.) kwa kazi yake kuhusu "Syntax of infinitival formations in the Indo-European languagues". Tangu 1977 mpaka 1990 alifanya kazi nyingine kama mwanamaarifa na alifanya madarasa katika Berlin, Vienna na Salzburg. Mwaka wa 1991, alipofanya kazi kama mwanamaarifa kwa isimu ya mashariki ya kompyuta, yeye alifanya habilitation katika chuo kikuu mji wa Bamberg kwa kazi yake kuhusu "Iranian loanwords in Armenian and Georgian". Jost Gippert afundisha isimu ya mlingo katika chuo kikuu "Johann-Wolfgang-Goethe", Frankfurt, tangu 1994. Tangu 1996 yeye ni mwanachama mgeni wa „Gelati Science Academy“ (Georgia). Tangu 2002 yeye ni mwanachama wa "Tufankommission"; na tangu 2007 ni mwanachama wa Katikati "Lugha" ya Chuo cha Sayansi Berlin-Brandenburg (Berlin-Brandenburg Science Academy).
Mwaka wa 1997 aliteuwa profesa wa heshima katika chuo kikuu "Sulkhan Saba Orbeliani", mji wa Tbilisi (Georgia), na 2009 aliteuwa udaktari wa heshima katika chuo kikuu "Ivane Javakhishvili", mahali sawasawa. Na mwaka wa 2013 aliteuwa udaktari wa heshima katika chuo kikuu "Shota Rustaveli", mji wa Batumi (Georgia). Kazi zake muhimu kama profesa kwa isimu ya mlingo katika Frankfurt, licha ya uchunguzi wa lugha za Kihindi-Kiulaya na mgawanyiko jenerali wa lugha, ni uchunguzi wa lugha za Caucasus. Miradi mingine ya kimataifa imefanyiwa chini ya usimamizi wake.
Jost Gippert anatawala mradi wake "TITUS" kama mwanaisimu wa kompyuta tangu mwaka 1987. Mradi "TITUS" wana shabaha kubomba madata ya nakala ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Uchunguzi muhimu wa Jost Gippert ni isimu ya mlingo na kihistoria, mgawanyiko ya lugha, electronic text corpora, multimedia language documentation na electronic manuscript analysis.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Jost Gippert, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.