Johann Wolfgang Von Goethe

Johann Wolfgang von Goethe alikuwa mwandishi, mshairi, mwanasiasa, mwanafalsafa na mwanasayansi Mjerumani anayekumbukwa kama mwandishi mkuu katika fasihi ya Ujerumani.

Johann Wolfgang Von Goethe
Goethe alivyochorwa mwaka 1828

Alizaliwa mjini Frankfurt am Main tar. 28 Agosti 1749 akafa Weimar 22 Machi 1832. Alisoma sheria lakini alianza kuandika riwaya za kwanza akiwa mwanafunzi.

Waziri mjini Weimar

1775 alipewa kazi ya mshauri wa mtemi wa Sachsen-Weimar na mwaka uliofuata alikuwa waziri katika serikali ya mtemi. Katika miaka ya utumishi wake alishughulika idara nyingi tofauti kama jeshi, fedha, ujenzi wa barabara na elimu. Wakati wake mji mdogo wa Weimar ilipata sifa kubwa ikatembelewa na wageni kutoka Ulaya wote waliotaka kumwona Goethe na Weimar ilikuwa kama kitovu cha utamaduni cha Ujerumani.

Aliendelea kuandika mengi kama riwaya, tamthiliya na mashairi. Tamthiliya ya "Faust" imekuwa kazi yake kuu.

Kazi za kisayansi

Pamoja na kuandika alianza kujishughulisha na sayansi. Alipenda sana sayansi mpya za biolojia na kemia. Kama waziri alianzisha idara ya kwanza ya kemia ya Ulaya kwenye chuo kikuu cha Jena.

Alifanya utafiti kwenye mifupa ya kiunzi cha mwili akatambua mfupa mmoja kichwani kisichojulikana bado. Aliandika pia kuhusu maumbo ya mimea akajenga misingi ya uainishaji wa kisayansi.

Katika fizikia alitunga nadharia juu ya rangi inayoendelea kujadiliwa kati ya wataalamu hadi leo.

Johann Wolfgang Von Goethe 
Sanamu ya Goethe mjini Heidelberg

Viungo vya Nje

Johann Wolfgang Von Goethe 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:

Tags:

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Jakaya KikweteOrodha ya wanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoLugha ya taifaWingu (mtandao)Dubai (mji)Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoNamba za simu TanzaniaMahakama ya TanzaniaUchaguziMwaniHistoria ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoSayansiOrodha ya milima ya AfrikaRohoSteve MweusiDubaiMuhimbiliMaandishiJulius NyerereKitenzi kikuu kisaidiziDhamiraBikiraKanisaFananiUnyenyekevuRisalaMzabibuMoscowMkoa wa MbeyaMfumo katika sokaMoyoMazingiraMshororoJacob StephenNdoa katika UislamuOrodha ya Marais wa MarekaniNenoIsimuTanganyikaWakingaMimba za utotoniMkuu wa wilayaMisemoC++MbeyaPunda miliaKanda Bongo ManMkoa wa KageraWagogoKamusiMtakatifu MarkoSensaRitifaaAthari za muda mrefu za pombeMaana ya maishaMkoa wa ArushaWahayaNimoniaNileWashambaaUhuru wa TanganyikaBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiTarafaUtumbo mpanaFonolojiaWarakaMunguUpendoTanganyika (ziwa)PamboVihisishiUzazi wa mpangoMlongeMtaalaKifua kikuu🡆 More