Hindu Kush ni safu ya milima ya kunjamano katika Asia ya Kati.
Inaenea kuanzia Afghanistan upande wa magharibi hadi Pakistan na kuishia katika China na Tajikistan.
Mlima wa juu ni Tirich Mir wenye kimo cha mita 7,708.
Njia za kuvuka milima hiyo ziko kwenye mipito ya Mintaka, Kilik, Chilinji na Kuramber zikiunganisha Kashmir na nchi za Asia ya Kati.
Mito mingi pamoja na Chapursan, Ishkuman, Ghizar, Gilgit na Shandur hutoka kwenye mabonde ya Hindu Kush na mwishowe hujiunga na Mto Indus. Upande wa kaskazini maji ya Hindu Kush hutiririka kuingia katika mto Amu Darya.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Hindu Kush kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Hindu Kush, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.