Hela

Hela ni jina kwa pesa lililo kawaida katika Tanzania.

Asili ya neno ni lugha ya Kijerumani. "Heller" ilikuwa kitengo cha pesa ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani au Tanzania bara kuanzia 1904 hadi 1918. Waingereza baada ya kuchukua utawala wa koloni walibadilisha sarafu kuwa shilingi na senti lakini jina la "hela" lilibaki kwa ajili ya pesa kwa jumla.

Hela
Heller ya 1913 (mbele)
Hela
Heller ya 1913 (nyuma)

Heller ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani

Tangu 1904 serikali ya Ujerumani ilichukua wajibu wa kutoa pesa kwa koloni yake katika Afrika ya Mashariki iliyojumlisha Tanzania bara pamoja na Rwanda na Burundi. Hadi mwaka ule Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki iliendelea kutoa sarafu yake iliyokuwa rupie 1 yenye pesa 64. Serikali ilipochukua jukumu hii iliamua kuendelea na rupie lakini ilibadilisha vitengo vyake vidogo kuwa Heller 100. Heller iliwahi kuwa pesa ndogo ya kihistoria katika Ujerumani lakini haikutumiwa tena tangu maungano ya Ujerumani mwaka 1871 na kuanzishwa kwa pesa ya kitaifa ya Mark na Pfennig.

Sarufi za Heller za Afrika ya Mashariki zilionyesha upande wa mbele neno "Heller" na namba ya thamani yake; upande wa nyumba ilikuwa na taji la Kaisari, maneno ya "Deutsch Ostafrika" (Afrika ya Mashariki ya Kijerumani) na mwaka wa kutolewa.

Heller ya Afrika ya Mashariki ilitolewa kwa sarufi za

Heller za Ulaya

Asili ya pesa iliyoitwa "heller" ni mji wa Kijerumani wa Hall inayoitwa leo Schwäbisch Hall. Kule sarafu za fedha zilitolewa tangu mwaka 1288 zilizosambaa haraka zikaitwa "Haller" au "Heller" kutokana na jina la mji. Polepole kiasi cha fedha ndani ya sarafu kilipungukiwa hadi kuwa sarafu ya shaba yenye thamani ndogo.

Heller iliendelea kuwa sarafu ndogo ya kawaida (kama senti) katika Ujerumani hadi mwaka 1873 ilipofutwa baada ya kuanzishwa kwa fedha mpya ya Mark na Pfennig. Austria-Hungaria iliendelea kuitumia kama sarafu ndogo ya Krone hadi mwisho wa dola hili. Chekoslovakia kama nchi mojawapo iliyotokana na Austria-Hungaria ilikuwa nchi ya pekee kuendelea na sarafu hii kwa jina "haler". Baada ya kugawiwa kwa Chekoslovakia kuwa nchi mbili za Ucheki na Slovakia zote mbili zilkuwa na haler hadi kujiunga na Euro.

Tags:

Afrika ya Mashariki ya KijerumaniPesaShilingiTanzania

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

SiasaDiamond PlatnumzMbeya (mji)Wizara ya Mifugo na UvuviBarua pepePapaMuundoLionel MessiUsawa (hisabati)vvjndNomino za kawaidaDaudi (Biblia)TabataNabii EliyaUzalendoVirusi vya UKIMWIKondomu ya kikeBikiraMagonjwa ya machoTawahudiChristopher MtikilaVita vya KageraSaidi Salim BakhresaRushwaLiverpool F.C.Maajabu ya duniaKoloniMkoa wa KigomaNamba tasaAlizetiFananiPapa (samaki)Orodha ya Marais wa ZanzibarMichezoUnyenyekevuNguzo tano za UislamuOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaMkoa wa SimiyuMsokoto wa watoto wachangaMr. BlueTumbakuOrodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watuStadi za maishaMwamba (jiolojia)Julius NyerereFonolojiaHistoria ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoYesuNileDar es SalaamMvuaKishazi tegemeziViwakilishi vya pekeeMaishaAlama ya barabaraniIsimuKenyaUkabailaIsraeli ya KaleHoma ya matumboJokofuOrodha ya nchi kufuatana na wakaziMartha MwaipajaUpinde wa mvuaMarie AntoinetteRoho MtakatifuShetaniMkoa wa Dar es SalaamSikukuu za KenyaSinagogiBahari ya HindiSoko la watumwaKidole cha kati cha kandoUgonjwa wa kuharaOrodha ya Watakatifu WakristoBendera ya Tanzania🡆 More