Utaifa ni itikadi ya mtu kupenda taifa lake kupita kiasi, hata kudharau watu wa mataifa mengine.
Hivyo ni tofauti na uzalendo unaomfanya mtu apende nchi yake kwa kutambua mema mengi aliyopata kutoka kwake.
Mara nyingi unajitokeza pia kama dharau kwa wananchi walio tofauti na kawaida kwa utamaduni, lugha n.k.
Katika ngazi ya chini, tunakuta ukabila.
Bendera ya taifa, wimbo wa taifa na alama nyingine za utambulisho ni muhimu katika kuchochea uzalendo, lakini mara nyingine zinachangia utaifa.
Elimunafsia inaeleza kwamba pendo kwa taifa linatokana na haja ya kuhusiana na wengine, lakini ni tofauti na mapendo mengine, k.mf. pendo kwa dini au kwa mchumba.
Kwa vyovyote ukomavu unadai mtu ajali wenzake asiwaone kama maadui kwa sababu tu ni tofauti naye.
|date=
(help)|date=
(help)|date=
(help)Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Utaifa, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.