Wavikingi

Wavikingi ni jina la kujumlisha makundi ya watu wa makabila ya Kigermanik katika Ulaya ya Kaskazini walioonekana kwa majirani kama wafanyabiashara na pia maharamia wa baharini.

Wavikingi
Upanuzi wa Waskandinavia wakati wa karne za 8 - 11

Asili yao ilikuwa katika Skandinavia ya Kaskazini na kusini, wakatumia jahazi ndogo wakivuka nazo Bahari ya Kaskazini, Bahari ya Baltiki na kuingia pia barani kupitia mito ya Ulaya hadi Mediteranea.

Mara nyingi walishambulia tu miji na vijiji vya pwani wakipora mali na kurudi kwao.

Kulikuwa pia na vipindi ambako Wavikingi walifaulu kuteka eneo fulani na kukaa huko. Walifika Uingereza, Uskoti, Ufaransa, Hispania, Urusi hadi Bizanti na Sisilia.

Katika Uingereza, Ufaransa ya Kaskazini na Italia ya Kusini walianzisha makazi wakitawala maeneo huko kwa muda. Huko walijulikana pia kwa majina kama Wanormani au Rus, na Rus ndiyo asili ya jina la Urusi.

Walivuka pia Atlantiki na kufika Greenland na Kanada.

Walihofiwa mara nyingi kama majambazi wakali lakini walitafutwa pia kama wanajeshi wa kukodi.

Inaaminiwa ya kwamba waliondoka kwao kwa sababu hali ya hewa ilileta njaa na uhaba wa ardhi ya kulima na pia kwa sababu utajiri wa nchi za kusini iliwavuta vijana wao.

Wavikingi
Jahazi ya Wavikingi

Viungo vya Nje

Wavikingi 
Wiki Commons ina media kuhusu:
Wavikingi  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wavikingi kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

BahariHaramiaJinaKabilaKigermanikKundiUlaya ya KaskaziniWafanyabiasharaWatu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

MzeituniLady Jay DeeMpira wa miguuKinembe (anatomia)MariooJokate MwegeloUbaleheTamthiliaMbadili jinsiaMpira wa mkonoZakaOrodha ya nchi kufuatana na wakaziSaidi NtibazonkizaTafsiriNembo ya TanzaniaMapambano ya uhuru TanganyikaKanisaViwakilishi vya kuoneshaKondomu ya kikeMziziMbogaPamboKanye WestKunguruMichael JacksonChakulaMbuga za Taifa la TanzaniaMlongeYesuShukuru KawambwaTambikoSteven KanumbaMusaVidonda vya tumboWayahudiSanaaNamba tasaWimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiPemba (kisiwa)Ala ya muzikiUtumbo mpanaMasafa ya mawimbiBunge la TanzaniaAli KibaLuhaga Joelson MpinaVieleziUajemiOrodha ya viongoziMkoa wa KigomaMkoa wa LindiLakabuOrodha ya mito nchini TanzaniaUchumiBiolojiaKimara (Ubungo)Kishazi tegemeziMadhara ya kuvuta sigaraWilaya ya KinondoniMaudhui katika kazi ya kifasihiMiundombinuMbaraka MwinsheheHistoria ya WapareAzimio la ArushaVivumishi vya kuoneshaMafurikoYoung Africans S.C.MwakaKutoa taka za mwiliKilimanjaro (volkeno)Kutoka (Biblia)VihisishiMkunduTenzi tatu za kale🡆 More