Vaginosisi Inayosababishwa Na Bakteria

Vaginosisi inayosababishwa na bakteria (kifupisho cha Kiingereza: BV; pia inajulikana kama bakteriosisi ya uke au Vaginitisi ya gadinerela, ni ugonjwa wa uke unaosababishwa na wingi wa bakteria.

Vaginosisi inayosababishwa na bakteria
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyGynaecology Edit this on Wikidata
ICD-10B96., N76.
ICD-9616.1
MeSHD016585

Dalili za kawaida ni pamoja na ongezeko la mchozo wa uke ambao mara nyingi hutoa harufu ya samaki. Mchozo huu huwa wa rangi nyeupe au ya kijivu. Kuchomwa na mkojo ni hali inayoweza kutokea. Kuwashwa huwa kwa nadra. Mara kwa mara, hali hii huwa bila dalili.

Uwepo wa BV huongeza hatari ya maambukizi ya maradhi ya zinaa ikiwa ni pamoja na VVU/UKIMWI. Hali hii pia huongeza hatari ya kujifungua kabla ya wakati miongoni mwa wanawake wajawazito.

Kisababishi na utambuzi

BV husababishwa na ukosefu wa uwiano wa bakteria asilia ukeni. Kuna mabadiliko katika aina ya bakteria inayotokea mara nyingi zaidi na ongezeko la mia hadi elfu moja ya idadi jumla ya bakteria zilizopo. Vipengele vya hatari hujumuisha kupiga bomba, wapenzi wapya au wengi, antibiotiki, na kutumia kifaa cha kuingiza ndani ya uterasi. Hata hivyo, ugonjwa huu hauainishwi kama ugonjwa wa zinaa. Utambuzi hukisiwa kwa msingi wa dalili na unaweza kuthibitishwa kwa kupima mchozo wa uke na kutambua viwango vya juu kuliko kawaida vya pH ya ukeni na idadi kubwa ya bakteria. Mara nyingi BV hudhaniwa kuwa maambukizi ya chachu ya ukeni au maambukizi ya Trikomonasi.

Kinga na tiba

Kwa kawaida, matibabu huwa ya antibiotiki, clindamycin au metronidazole. Dawa hizi pia zinaweza kutumika katika trimesta ya pili au ya tatu ya ujauzito. Hata hivyo, mara nyingi hali hii hurejea baada ya kutibiwa. Probiotiki zinaweza kusaidia kuzuia kurejea kwa hali hii. Haijulikani bayana kama kutumia probiotiki au antibiotiki huathiri matokeo ya ujauzito.

Epidemiolojia na historia

BV ni maambukizi ya uke yanayotokea mara nyingi katika wanawake wa umri wa kuzaa. Idadi ya wanawake wanaoathiriwa katika muda fulani ni kati ya asilimia 5 na asilimia 70. BV hutokea mara nyingi zaidi katika maeneo mengi ya Afrika na ni nadra barani Asia na Ulaya. Nchini Marekani, takriban asilimia 30 ya wanawake wa umri wa kati ya miaka 14 na 49 huathiriwa. Viwango hutofautiana sana katika makundi ya kikabila mbalimbali katika nchi. Ingawa BV kama dalili imeainishwa katika kipindi kirefu cha historia, nakala za kwanza bayana ziliwekwa katika mwaka wa 1894.

Marejeo

Viungo vya nje

Vaginosisi Inayosababishwa Na Bakteria  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vaginosisi inayosababishwa na bakteria kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Vaginosisi Inayosababishwa Na Bakteria Kisababishi na utambuziVaginosisi Inayosababishwa Na Bakteria Kinga na tibaVaginosisi Inayosababishwa Na Bakteria Epidemiolojia na historiaVaginosisi Inayosababishwa Na Bakteria MarejeoVaginosisi Inayosababishwa Na Bakteria Viungo vya njeVaginosisi Inayosababishwa Na BakteriaBakteriaKifupishoKiingerezaUgonjwaUke

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Bendera ya TanzaniaUhifadhi wa fasihi simuliziMfumo wa homoniYoung Africans S.C.Mkoa wa ShinyangaMaradhi ya zinaaTelevisheniShambaSaidi Salim BakhresaVita Kuu ya Pili ya DuniaApril JacksonDaktariNathariNguzo tano za UislamuSinagogiIsimuSadakaMauaji ya kimbari ya RwandaKukuMkoa wa SongweUmoja wa MataifaVita Kuu ya Kwanza ya DuniaMvuaWangoniArsenal FCTafsiriMweziFred MsemwaHistoria ya UislamuKitenzi kikuu kisaidiziKambaleHistoria ya BurundiWilaya ya IlalaArudhiTungo kiraiWingu (mtandao)Ufugaji wa kukuMkoa wa MaraMsichanaKengeSeli nyekundu za damuMkoa wa Unguja Mjini MagharibiFasihiMisriKamusi za KiswahiliVitendawiliMaudhui katika kazi ya kifasihiMafumbo (semi)Wataru EndoMajira ya mvuaOrodha ya Marais wa BurundiOrodha ya Makamu wa Rais TanzaniaIdara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)Sahara ya MagharibiHalmashauriNguruweMaeneo ya Kihistoria ya Kitaifa ya TanzaniaOrodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifaMkoa wa DodomaSteve MweusiNetiboliInshaMapenzi ya jinsia mojaWokovuImaniRedioNafsiVipaji vya Roho MtakatifuMatendo ya MitumeTabianchiMwaka wa KanisaPaul MakondaJiniWanyaturu🡆 More