Sanzawa

Sanzawa ni kata ya Wilaya ya Chemba katika Mkoa wa Dodoma, Tanzania, yenye postikodi namba 41811.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 15,970 . Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 10613 waishio humo.

Sanzawa ipo katika tarafa ya Kwamtoro. Ina jumla ya vitongoji vinane. Wakazi wake ni wasandawe, wagogo na wabarabaig. Wakazi wa Sanzawa wanajishughulisha na kilimo cha mazao ya chakula na biashara. Mazao ya chakula ni pamoja na mahindi, uwele, mtama, udo, mihogo n.k. Mazao ya biashara ni alizeti, ufuta na karanga.

Wakazi wa Sanzawa pia ni wafugaji wa mifugo mbalimbali. Hali ya hewa ya Sanzawa ni nusu jangwa hivyo hukabiliwa na ukame na hali ya ukosefu wa maji kwa kipindi kirefu. Hivyo kwa wafugaji hutembea umbali mrefu kutafuta maji kwa ajili mifugo yao.

Sanzawa pia ni makao makuu ya kata. Hivyo ina shule ya sekondari ya kata.

Marejeo

Sanzawa  Kata za Wilaya ya Chemba - Mkoa wa Dodoma - Tanzania Sanzawa 

Babayu | Chandama | Chemba | Churuku | Dalai | Farkwa | Goima | Gwandi | Jangalo | Kidoka | Kimaha | Kinyamsindo | Kwamtoro | Lahoda | Lalta | Makorongo | Mondo | Mpendo | Mrijo | Msaada | Ovada | Paranga | Sanzawa | Songolo | Soya | Tumbakose


Sanzawa  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Dodoma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Sanzawa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

Tags:

KataMkoa wa DodomaNambaPostikodiTanzaniaWilaya ya Chemba

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Mohamed HusseinLughaUandishiMjasiriamaliUkristoMnyoo-matumbo MkubwaUingerezaBob MarleyKiongoziDhahabuUtendi wa Fumo LiyongoSakramentiMoyoWagogoTungoJulius NyerereDiego GraneseAli Hassan MwinyiUsanisinuruZiwa ViktoriaUkraineOrodha ya Magavana wa TanganyikaDubai (mji)Samia Suluhu HassanMarie AntoinetteMalaikaKito (madini)Ufahamu wa uwezo wa kushika mimbaMasharikiBabeliDiplomasiaJinsiaInsha ya wasifuUenezi wa KiswahiliUmoja wa AfrikaSubrahmanyan ChandrasekharHistoria ya TanzaniaZuhuraJamhuri ya Watu wa ZanzibarMaana ya maishaMsamiatiUislamu kwa nchiUtamaduniTheluthiOrodha ya milima mirefu dunianiKaizari Leopold ISayariKarne ya 20PamboMohammed Gulam DewjiKata za Mkoa wa MorogoroUzazi wa mpango kwa njia asiliaKibonzoMandhariMagavanaBarua pepeViwakilishi vya sifaHisabatiFasihi andishiMimba za utotoniTahajiaUrusiKilimoHuduma ya kwanzaMofolojiaMfumo katika sokaHektariUgonjwa wa uti wa mgongoMuda sanifu wa duniaAgano la KaleMbeya (mji)WWaarabuFonimuDiraVivumishi vya idadiBikira MariaDiamond Platnumz🡆 More