Raphael

Raffaello Sanzio (kwa Kiitalia huitwa pia Raffaello da Urbino; kwa Kiingereza anajulikana kama Raffael au Raphael) (6 Aprili 1483 - 6 Aprili 1520) alikuwa mchoraji na mjenzi kutoka Italia.

Raphael
Raphael alivyojichora.

Pamoja na Leonardo da Vinci na Michelangelo huhesabiwa kati ya wasanii muhimu wa zama ya mwamko ya Italia.

Maisha

Raphael alizaliwa mjini Urbino kama mtoto wa mchoraji Giovanni Santi aliyefanya kazi katika utumishi wa mkabaila Federiko III wa Montefeltro.

Katika umri wa miaka 15 alikuwa mwanafunzi katika karakana ya mchoraji Pietro Perugino aliyeshiriki katika kazi za kupamba Kikanisa cha Sistina kwenye Vatikano.

Raphael alijifunza haraka na tangu mwaka 1500, alipokuwa na umri wa miaka 17, alipewa kazi za kwanza za kujitegemea.

Alianza kuchora picha katika makanisa ya miji mbalimbali ya Italia.

Alipenda kutembelea Firenze akitazama michoro ya walimu wa kale.

Tangu alipohamia Roma, alikoitwa na Papa Julius II, kazi kubwa aliyopewa ilikuwa picha za ukutani kwenye vyumba vya Papa mwenyewe.

Raphael aliaga dunia mapema katika umri wa miaka 37. Hakuoa wala hakuna watoto waliojulikana.

Upande wa dini, alikuwa Mkristo wa Kanisa Katoliki, tena mwanachama wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko.

Michoro yake

Viungo vya nje

Raphael  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Raphael kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

148315206 ApriliItaliaKiingerezaKiitaliaMchorajiMjenzi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

JipuKendrick LamarMawasilianoUtafitiOrodha ya Maspika wa Bunge la TanzaniaMivighaNyasa (ziwa)Manchester CityVielezi vya mahaliUturukiAfrikaAfrika Mashariki 1800-1845SalaMachweoKamusi ya Kiswahili sanifuJuxPalestinaTamthiliaOrodha ya viongoziLigi ya Mabingwa AfrikaIsraeli ya KaleOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaJamhuri ya Watu wa ZanzibarDamuDakuInsha ya wasifuJotoMlongeAnna MakindaKahawiaOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaIdara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)UpepoRushwaLahaja za KiswahiliBustani ya EdeniTetekuwangaOrodha ya vyama vya siasa TanzaniaBenjamin MkapaSimba S.C.Mtandao wa kompyutaHifadhi ya SerengetiMapigo yasiyo ya kawaida ya moyoNafsiJuma kuuTanzania Breweries LimitedTanganyika (ziwa)Historia ya Kanisa KatolikiAngahewaVichekeshoMvuaKaramu ya mwishoWanyama wa nyumbaniMnyamaHomanyongo CBawasiriNyweleKipaimaraJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaSenegalUbongoWizara za Serikali ya TanzaniaShairiMwanamkeLigi Kuu Uingereza (EPL)Maambukizi ya njia za mkojoUkimwiDiamond PlatnumzTungo kishaziUchawiViwakilishi vya urejeshiKibodiBata MzingaRohoLughaSiku tatu kuu za PasakaKima (mnyama)🡆 More