Nge

Kwa matumizi tofauti ya jina hili angalia Akarabu (kundinyota)

Nge
Nge mkia-mnene manyoya (Parabuthus villosus) akionyesha magando na msumari yake
Nge mkia-mnene manyoya (Parabuthus villosus) akionyesha magando na msumari yake
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Faila: Arthropoda
Nusufaila: Chelicerata
Ngeli: Arachnida
Nusungeli: Dromopoda
Oda: Scorpiones
Ngazi za chini

Familia za juu 6:

  • Buthoidea
  • Chaeriloidea
  • Chactoidea
  • Iuroidea
  • Pseudochactoidea
  • Scorpionoidea

Nge au akrabu (kutoka Kiarabu عقرب) ni arithropodi wa oda Scorpiones katika ngeli Arachnida. Spishi ndogo huitwa visusuli pia. Kama arakinida wote wana miguu minane. Pedipalpi zao ni kubwa na zina gando, na mkia ni mrefu na una msumari mkubwa mwishoni kwake. Kama kawaida kiwiliwili chao kina sehemu mbili: kefalotoraksi ( cephalothorax: kichwa na kidari) na fumbatio lakini zimeungwa vipana, siyo kwa pediseli (pedicel) nyembamba kwa umbo wa mrija kama kwa buibui. Mgongo wa kefalotoraksi ni mgumu na kwa hivyo huitwa gamba (carapace). Nge wana macho 6-12, mawili juu ya gamba la kefalotoraksi na 2-5 kwa kila upande wa kichwa. Msumari wa nge hutumika kwa kudunga windo na kuingiza sumu ndani yake. Windo akiwa amekufa, kelisera (chelicerae) za nge zinakata vipande vidogo vinavyowekwa katika kishimo mbele ya mdomo. Maji ya umeng'enyaji yakamuliwa katika kishimo hiki na baada ya kumeng'enya chakula myeyuko ufyondwa. Nge hula arithropodi wengine na wale wakubwa hula mijusi na vipanya wadogo pia.

Spishi zilizochaguliwa za Afrika ya Mashariki

  • Babycurus gigas
  • Babycurus wituensis
  • Buthotus emini
  • Buthotus trilineatus
  • Hottentotta trilineatus
  • Iomachus politus
  • Isometrus maculatus
  • Lychas asper
  • Lychas burdoi
  • Odonturus dentatus
  • Opisthacanthus fischeri
  • Opistophthalmus glabrifrons
  • Pandinus bellicosus
  • Pandinus viatoris
  • Parabuthus liosoma
  • Parabuthus pallidus
  • Uroplectes fischeri

Picha

Tags:

Akarabu (kundinyota)

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Unju bin UnuqJinaKisononoRihannaMbuga za Taifa la TanzaniaMatendeOrodha ya makabila ya TanzaniaOrodha ya viongoziHistoria ya WapareMaghaniMkanda wa jeshiUfugaji wa kukuVichekeshoKuraniOrodha ya Marais wa ZanzibarMwenge wa UhuruUkoloniMafua ya kawaidaMitume na Manabii katika UislamuMkoa wa KataviAfrika ya MasharikiUyahudiMkoa wa ManyaraBarabaraWasukumaMkoa wa Unguja Mjini MagharibiNyegereReal BetisBawasiriMkoa wa MtwaraHekalu la YerusalemuAndalio la somoKendrick LamarMjombaUfahamuMarekaniAsili ya KiswahiliKidole cha kati cha kandoKadi ya adhabuUpinde wa mvuaIdara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)PesaKinembe (anatomia)ShairiMbiu ya PasakaKiumbehaiMtaalaRamaniChelsea F.C.KiraiWilaya za TanzaniaJihadiLil Wayne28 MachiWiki CommonsKima (mnyama)Ngome ya YesuAli Hassan MwinyiPichaKiboko (mnyama)PalestinaAJokate MwegeloKiambishi2 AgostiUfufuko wa YesuMlongeOrodha ya shule nchini TanzaniaChuo Kikuu cha Dar es SalaamVidonge vya majiraOrodha ya wanamuziki wa AfrikaIntanetiAfyaMalariaDizasta VinaChama cha Mapinduzi🡆 More