Neopalpa Donaldtrumpi

Neopalpa donaldtrumpi ni spishi ya nondo iliyogunduliwa mwaka 2017 na mtaalamu wa Kanada Vazrick Nazari.

Neopalpa donaldtrumpi
Kichwa cha Neopalpa donaldtrumpi kwa kuitazama kutoka upande wa kushoto na mbele.
Kichwa cha Neopalpa donaldtrumpi kwa kuitazama kutoka upande wa kushoto na mbele.
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Lepidoptera (Wadudu walio na mabawa wenye vigamba)
Familia: Gelechiidae
Jenasi: Neopalpa
Spishi: N. donaldtrumpi
Nazari, 2017

Akiwa mgunduzi wa spishi mpya Nazari aliweza kuchagua jina akaamua kutumia jina la mwanabiashara na wakati ule mgombea wa uraisi Donald Trump kwa matumaini ya kwamba chaguo hili litasababisha watu wengi zaidi kusikia habari za wadudu na utafiti wa wadudu.

Ugunduzi

Neopalpa Donaldtrumpi 
Donald Trump akionyesha nywele zake za ajabu

Jenasi Neopalpa pamoja na spishi Neopalpa neonata ilielezwa mara ya kwanza mwaka 1998 na Dalibor Povolný. Miaka 20 baadaye Vazrick Nazari aliangalia upya mifano ya kipepeo hiki iliyohifadhiwa katika taasisi ya Bohart Museum of Entomology. Alitambua ya kwamba mifano kadhaa ilitofautiana na mingine na kuwa spishi mpya aliyoiita Neopalpa donaldtrumpi kwa sababu ya vigamba vya rangi ya njano-nyeupe kichwani. Haya yalimkumbusha kuhusu nywele za Donald Trump. Ilhali nafasi yake ya kueleza spishi mpya ilitokea karibu na tarehe ya Trump kuingia katika uraisi kwenye januari 2017 aliamua kutumia hili kwa sababu aliona sayansi ya wadudu ilihitaji kujulikana zaidi.

Tabia

Mwili wa kipepeo hiki una urefu baina ya milimita 7 na 13. Mabawa yake hufunika upana wa milimita 6 hadi 9.2. Uso wa juu wa mabawa huwa na rangi kahawia pamoja na madoa meupe zaidi. Kichwa kina vigamba vyeupe-njano yaliyosababisha uteuzi wa jina. Pamoja na vigamba vya kichwani tofauti nyingine ya spishi hii na spishi ya N. neonata ni udogo wa mboo na pia umbo la sehemu za kike. Zinatofautishwa pia kutokana na DNA.

Makazi

Hadi sasa Neopalpa donaldtrumpi ilionekana kwenye sehemu za kaskazini ya rasi ya Baja California katika Meksiko na kwenye kaskazini ya Kalifornia ya Marekani.

Marejeo

Viungo vya Nje

Neopalpa Donaldtrumpi 
Wiki Commons ina media kuhusu:

Tags:

Neopalpa Donaldtrumpi UgunduziNeopalpa Donaldtrumpi TabiaNeopalpa Donaldtrumpi MakaziNeopalpa Donaldtrumpi MarejeoNeopalpa Donaldtrumpi Viungo vya NjeNeopalpa DonaldtrumpiDonald TrumpKanadaNondoSpishiWadudu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

KiumbehaiFananiUtamaduni wa KitanzaniaNguvuKipanya (kompyuta)Ngono KavuKifua kikuuNomino za jumlaUgonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaViunganishiKunguniInshaHakiNomino za wingiSitiariVivumishi vya -a unganifuOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaWagogoJamiiVidonda vya tumboUnyenyekevuTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya TanzaniaVitenzi vishiriki vipungufuMrisho NgassaNguruweSalaUtumbo mpanaKisononoMajiMaambukizi ya njia za mkojoJohn Raphael BoccoMjasiriamaliMbeya (mji)Chombo cha usafiri kwenye majiKitufeMkoa wa ArushaFutiNadhariaMkoa wa PwaniHistoria ya KiswahiliVivumishi vya urejeshiAbedi Amani KarumeKiambishi tamatiHomoniChadMwanzo (Biblia)Mwanga wa juaMsamiatiTheluthiLughaMkoa wa Dar es Salaam13LenziBogaAina za ufahamuThabitiMfupaHeshimaTanganyikaMalawiAmfibiaJiniAfrikaMazingiraLahaja za KiswahiliFani (fasihi)Historia ya ZanzibarKaizari Leopold IKoloniKukuSimbaRashidi KawawaMmea🡆 More