Mohamed Said

Mohamed Said Salum (alizaliwa Gerezani, Dar es Salaam, 25 Februari, 1952) ni mwandishi na mwanahistoria kutoka nchini Tanzania.

Ametunga vitabu mbalimbali, lakini anafahamika zaidi kwa kitabu chake cha "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes" kilichotolewa kwa lugha ya Kiingereza kwa mara ya kwanza 1998. Baadaye kikatafsiriwa kwa Kiswahili na kutolewa tena mnamo mwaka 2002.

Mohamed Said
Mohamed Said
Nyuma wapili Bakari Saleh, mwisho kulia Ilunga Hassan Kapungu,

Mstari wa mbele watatu kutoka kushoto Mwanahistoria - Mwandishi Mohamed Said. Hawa walikuwa baadhi ya vijana wa Kiislamu waliohudhuria Semina Dodoma Chuo Cha Biashara 1988.

Amezaliwa 25 Februari 1952 (1952-02-25) (umri 72)
Gerezani, Dar es Salaam
Nchi Tanzania
Kazi yake Mwandishi, mwanahistoria

Maisha na kazi

Sheikh Mohamed Said Abdallah alizaliwa mnamo tarehe 25 Februari katika mwaka wa 1952 huko Gerezani jijini Dar es Salaam - ambapo ndiko kulikokuwa na asili ya upinzani dhidi ya ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika. Babu yake, Mzee Salum Abdallah Popo alikuwa muasisi wa harakati za vyama vya wafanyakazi na alikuwa mmoja kati ya watu wa awali kabisa kuanzisha upinzani na kuunga mkono hoja ya kupinga utawala wa kikoloni. Mwaka wa 1947, Mzee Popo aliongoza mgomo wa kwanza nchini Tanganyika katika majimbo ya kati nchi uliopangwa na wafanyakazi wa Tanganyika Railways.

Tanganyika ilipopata uhuru wake mwaka 1961, Mzee Popo aliachana na mkono wa Nyerere kama jinsi wengi walivyofanya na alitiwa kizuizini na serikali kwa ajili ya msimamo wake wa kuwa vyama vya wafanyakazi sharti viwe huru. Akiwa mwenyekiti wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) alipinga vyama vya wafanyakazi kuwekwa chini ya Tanganyika African National Union (TANU) chini ya Rais Julius Nyerere.

Sheikh Mohamed Said ana shahada katika masuala ya Sayansi ya Siasa kutoka katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Vilevile ana Stashahada katika masuala ya Maritime Studies kutoka katika Chuo Kikuu cha Wales huko mjini Cardiff, Wales na nyingine ya BIMA kutoka katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha cha Dar es Salaam (IFM).

Utafiti juu ya historia ya uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said amefanya utafiti mwingi sana juu ya historia ya uhuru wa Tanganyika, historia ambayo kabla ya utafiti wake ilichukuliwa kama iliyohitimishwa na ameweza kufukua mambo muhimu ambayo yalifichwa katika historia iliyokuwa ikitambulikana rasmi.

Alianza kufahamika zaidi katika miaka ya themanini kupitia makala zake za kusisimua zilizokuwa zinahangaisha fikra za wasomaji kwa kufichua yale yaliyofichwam zilizoelezea mchango muhimu wa Waislamu na Uislamu katika harakati za kupinga ukoloni katika Tanganyika na khiyana waliofanyiwa Waislamu na serikali zote mbili, yaani, kabla ya uhuru na baada ya uhuru - jambo ambalo kwa wakati ule lilikuwa mwiko kufanyiwa utafiti au kuandikwa.

Makala hizo zilipata kuchapishwa katika magazeti na majarida maarufu barani Afrika na katika magazeti ndani na nje ya Tanzania. Baadhi tu ya makala zake za utafiti ni pamoja na "In Praise of Ancestors" (1988), "Africa Events (London), "Abdulwahid Sykes: Founder of a Political Movement" Africa Events - London (1988), "Islam and Politics in Tanzania" (1989), Al Haq Internation (Karachi), "The Plight of Tanzania Muslim" (1993) Change (Dar es Salaam) na "The Secular Unsecular State" (1995) Change (Dar es Salaam).


Tazama pia

Viungo vya Nje

Tags:

Mohamed Said Maisha na kaziMohamed Said Utafiti juu ya historia ya uhuru wa TanganyikaMohamed Said Tazama piaMohamed Said Viungo vya NjeMohamed Said19521998200225 FebruariDar es SalaamGerezaniKiingerezaKiswahiliLughaMaisha na Nyakati za Abdulwahid SykesMwakaMwanahistoriaMwandishiTanzaniaVitabu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Vivumishi vya kuoneshaPijiniMajiLiverpoolKutoka (Biblia)BurundiChristina ShushoNgano (hadithi)AVivumishi vya kumilikiKichecheNetiboliBiblia ya KikristoIsimuKonsonantiKata za Mkoa wa MorogoroMalengo ya Kiswahili kuwa lugha ya taifaSakramentiMsamahaUpendoKigoma-UjijiDawa za mfadhaikoMaajabu ya duniaKamusiUbongoNdiziOrodha ya Marais wa TanzaniaNdoaNguzo tano za UislamuMjombaUzalendoUtumwaMshubiriKoroshoMkoa wa MaraSemiUbadilishaji msimboSentensiGeorDavieMwana FARohoKanda Bongo ManUongoziNathariMkanda wa jeshiRayvannyMiundombinuDiamond PlatnumzVita Kuu ya Pili ya DuniaLionel MessiKataHadithi za Mtume MuhammadSerikaliKanye WestBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiHistoria ya WapareDalufnin (kundinyota)UajemiAndalio la somoUaUfugaji wa kukuKinyongaUandishi wa ripotiHaki za watotoBaraza la mawaziri TanzaniaHifadhi ya SerengetiMoyoKata za Mkoa wa Dar es SalaamRamaniMarekaniIsraelHistoria ya uandishi wa QuraniSayariHekaya za AbunuwasiSimba🡆 More