Mnavu au mnafu (Solanum nigrum) ni mmea katika familia Solanaceae.
Mnavu (Solanum nigrum) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mnavu | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Kwa kawaida huu ni mmea wa pori, lakini unapandwa mahali pengi katika Afrika ya Mashariki. Mingi ya mimea ya pori ina sumu, matunda mabichi hasa. Kula kwa beri bichi na mara nyingi majani pia kunaweza kusababisha kifo cha watoto na mifugo. Lakini aina za mnavu zinazopandwa zinaweza kuliwa baada ya kuzipika. Majani huuzwa kwa jina la manavu. Matunda mabivu yanaweza kuliwa kwa kawaida bila kupikwa, aina zenye matunda mekundu au yenye rangi ya machungwa hasa (rangi ya kawaida ni nyeusi).
Kuna spishi nyingine, Solanum americanum, ambayo imewasilishwa katika Afrika na ambayo inafanana sana na S. nigrum. Watu wengi hawawezi kulinganua spishi hizi na mbili zote huitwa mnavu. Hata S. americanum hulika.
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mnavu kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mnavu, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.