Milima ya kuvukia Antaktiki (kwa Kiingereza: Transantarctic Mountains) ni safu ya milima katika bara la Antaktiki.
Inagawa bara hilo kuwa sehemu mbili za mashariki na magharibi. Inaenea kwa zaidi ya km 3,200.
Miinuko ya juu ni zaidi ya mita 4,500 juu ya usawa wa bahari, mrefu zaidi ni Mlima Kirkpatrick (m 4528) katika Nchi ya Viktoria karibu na Bahari ya Ross. Miinuko ya juu zaidi zinaonekana juu ya ganda la barafu linalofunika bara lote lenye unene wa mita 3,000 lakini sehemu duni zaidi ya milima ziko chini ya uso wa barafu.
Rasi ya Antaktiki upande wa magharibi si sehemu ya milima hiyo.
Kutokana na baridi kali ya mazingira hakuna wanyama wala mimea: uhai pekee ni viumbehai sahili kama vile bakteria, mwani na kuvu.
Jina la "Transantarctic Mountains" ilitumiwa kwanza mnamo 1960, kwenye makala ya mtaalamu wa jiolojia Warren Hamilton.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Milima ya kuvukia Antaktiki, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.