Kidudu-Deraya

Familia 3:

Kidudu-deraya
Kidudu-Deraya
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Nusuhimaya: Eumetazoa
(bila tabaka): Bilateria
(bila tabaka): Prostomia
Faila ya juu: Ecdysozoa
Faila: Loricifera
Kristensen, 1983
Oda: Nanaloricida
Kristensen, 1983
Ngazi za chini

  • Nanaloricidae Kristensen, 1983
  • Pliciloricidae Kristensen & Higgins, 1986
  • Urnaloricidae Heiner & Kristensen, 2009

Vidudu-deraya ni wanyama wadogo sana wa bahari wa oda Nanaloricida, oda pekee ya faila Loricifera wanaofunikwa na mabamba kama deraya. Wana urefu wa mm 0.1-1. Huishi katika masimbi ya sakafu ya bahari kwa vina vyote, aina zote za masimbi na latitudo zote.

Wanyama hao wamefunua hivi karibuni kiasi. Faila yao imeelezewa mwaka 1983 na Kristensen. Mnamo 2021 spishi 43 zilikuwa zimeelezewa, lakini spishi nyingine 100 zinasalia kuelezewa.

Wana kiwiliwili kikubwa kilichozungukwa na mabamba sita ya deraya. Kichwa, ambacho hubeba miiba mingi iliyopinidika nyuma, huunganishwa na kiwiliwili kupitia shingo yenye pingili ambayo inaweza kurudishwa ndani ya deraya. Mdomo unaoweza kubenuliwa uko ncha ya mbele na umezungukwa na sindano nane. Ubongo umesitawi vizuri na umeunganishwa moja kwa moja na kila mwiba. Kamba ya neva hupita upande wa chini kuelekea ncha ya nyuma. Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula huanza na mfereji wa mdomo ambao unaweza kutolewa. Kisha hufuata koromeo ya umbo la tufe iliyo na misuli yenye nguvu na hatimaye utumbo ulionyooka ambao hufunguka katika mkundu mwishoni kabisa .

Picha

Marejeo

Tags:

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

AmfibiaMoyoMadhehebuMsamiatiKen WaliboraNomino za wingiTendo la ndoaUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaTeknolojiaMlongeMatumizi ya LughaShinikizo la ndani ya fuvuMkondo wa umemeManchester United F.C.Orodha ya Maspika wa Bunge la TanzaniaNandyShinikizo la juu la damuBiasharaDiraFarasiJamhuri ya KongoMkanda wa jeshiNyokaDaftariLugha za KibantuAUingerezaTeknolojia ya habariOrodha ya vitabu vya BibliaMenoLugha ya taifaMweziTausiWamanyemaWimboTai (maana)NyangumiRayvannyJangwaOrodha ya mito nchini TanzaniaUKUTASayari ya TisaFonolojiaNominoVielezi vya namnaSalama JabirMafua ya kawaidaHistoria ya UislamuKiarabuFananiIdi AminIsimuUtegemezi wa dawa za kulevyaKusiniPapaMsitu wa AmazonUgonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaMtakatifu PauloKishazi tegemeziMaharagweSilabiJulius NyerereKukuHoma ya matumboRadiHarmonizeOrodha ya viwanja vya michezo TanzaniaAsidiOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaThomas UlimwenguUfugaji wa kukuJipuVitenzi vishiriki vipungufuKarne ya 20Mkoa wa RukwaFIFABoga🡆 More