Kuoza Kwa Meno

Kuoza kwa meno (caries ni neno la Kilatini kutoka rottenness), pia hujulikana kama kuoza kwa jino, kaviti, au caries, ni kuharibika kwa meno kutokana na shughuli za bakteria.

Kaviti inaweza kuwa na aina tofauti za rangi kutoka kijani kibichi hadi nyeusi. Dalili zinaweza kujumuisha maumivu na ugumu wa kula chakula. Matatizo yanaweza kujumuisha inflamesheni ya tishu zinazozunguka jino, kupoteza jino, na maambukizi au usaha hutokea.

Kuoza kwa meno
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyUganga wa meno Edit this on Wikidata
ICD-10K02.
ICD-9521.0
DiseasesDB29357
MedlinePlus001055

Kisababishi

Bakteria huharibu tishu ngumu ya meno (enameli, dentini na sementamu) kwa kutengeneza asidi kutoka kwa mabaki ya chakula kwa sehemu ya jino. Sukari nyepesikatika chakula ni chanzo cha nguvu ya kimsingi ya bakteria na kwa hivyo lishe ya juu iliyo na sukari nyepesi ni swala la hatari. Ikiwa uharibifu wa madini ni mkubwa kuliko ujenzi kutoka kwa vyanzo kama vile mate, matokeo ni kuoza kwa meno. Maswala ya hatari inajumuisha hali zinazoleta matokeo ya mate kidogo kama vile: ugonjwa wa kisukari, Sindromu ya sjogren na baadhi ya matibabu. Matibabu yanayopunguza utoaji wa mate yanajumuisha antihistamines na dawa za kupunguza makali na mengine. Kuoza kwa meno pia kunahusishwa na umasikini usafishaji wa mdomo, na kurudi hali ya hapo awali ufizi wa meno inayoleta athari kwa mizizi ya meno.

Uzuiaji na matibabu

Uzuiaji hujumuisha: usafishaji wa meno kila wakati, lishe iliyo na sukari ya chini na kiwango kidogo cha floridi. Kupiga meno mswaki mara mbili kwa siku na kusafisha katikati ya meno mara moja kwa siku unapendekezwa na wengi. Floridi inaweza kutokana na maji, chumvi au dawa ya meno na vyanzo vinginevyo. Kutibu meno ya mama yaliyooza kunaweza kupunguza hatari kwa watoto wake kwa kupunguza idadi fulani ya bakteria. Uchunguzi unaweza kuleta utambuzi wa mapema. Kulingana na kiwango cha uharibifu, matibabu kadhaa yanaweza kutumika urejeshaji meno kwa hali yake ya kufanya kazi au jino linaweza kutolewa. Hakuna mbinu inayojulikana kurudia hali ya awali viwango vikubwa vya jino. Matibabu yaliyopo katika nchi zinazostawi ni duni kila mara. Paracetamol (acetaminophen) au ibuprofen inaweza kutumiwa kutuliza maumivu.

Epidemiologia

Kote duniani, takribani watu bilioni 2.43 (asilimia 36 ya idadi ya watu)  wana meno yaliyooza ya kudumu. Shirika la Afya Duniani linakadiria kuwa karibu watu wote wazima huwa na meno yaliyooza kwa wakati fulani. Meno ya watoto wachanga huathiri karibu watu milioni 620 au asilimia 9 ya idadi ya watu. Uozaji wa meno hutokea sana kwa watu wazima na watoto kwa miaka ya hivi karibuni. Ugonjwa huu unapatikana sana katika nchi zinazostawi na kiasi kwa nchi zilizostawi kwa sababu ya matumizi ya sukari kiasi.

Marejeleo

Tags:

Kuoza Kwa Meno KisababishiKuoza Kwa Meno Uzuiaji na matibabuKuoza Kwa Meno EpidemiologiaKuoza Kwa Meno MarejeleoKuoza Kwa MenoBakteriaJino

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

UNICEFUwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius NyerereWamandinkaMaghaniTabianchiOrodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifaPandaHassan bin OmariVielezi vya namnaFamiliaNgiriJamhuri ya Watu wa ZanzibarUrusiTetekuwangaMsukuleRisalaMnururishoNyokaNeemaShetaniKoreshi MkuuOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaKiboko (mnyama)MlongeUandishi wa ripotiSenegalTeknolojia ya habariKiunzi cha mifupaMfumo wa upumuajiAngkor WatSean CombsViwakilishiUgonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaTendo la ndoaNenoSteve MweusiMaishaSemiDNAVipera vya semiTabainiUkabailaHafidh AmeirMwaka wa KanisaMkoa wa KilimanjaroVivumishi vya -a unganifuIsraelLongitudoMji mkuuKaswendeWallah bin WallahMungu ibariki AfrikaMandhariMusaMamba (mnyama)MachweoTovutiUsawa (hisabati)UmaskiniMeliJacob StephenVasco da GamaWaluguruOrodha ya vitabu vya BibliaHijabuIsimujamiiSaharaWanyama wa nyumbaniLigi Kuu Tanzania BaraMadhara ya kuvuta sigaraWilaya ya Kilindi🡆 More