Koho

P.

Koho
Koho aliyekamata samaki
Koho aliyekamata samaki
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Accipitriformes (Ndege kama vipanga)
Familia: Pandionidae (Ndege walio na mnasaba na koho)
Jenasi: Pandion (Koho)
Savigny, 1809
Spishi: cristatus Vieillot, 1816

haliaetus Linnaeus, 1758

Koho ni ndege wakubwa kiasi wa jenasi Pandion, jenasi pekee ya familia Pandionidae. Zamani spishi moja tu ilifahamiwa, lakini bingwa kadhaa wamekupa nususpishi ya Australasia cheo cha spishi sasa na IOC (Muungano wa Kimataifa wa Wataalamu wa Ndege) unaiafiki. Lakini wataalamu wengine hawakubali.

Mwili wa koho ana sm 50-66 na upana wa mabawa ni sm 127-180. Mgongo wake una rangi ya kahawa na kidari na tumbo ni nyeupe. Mara nyingi kidari kina michirizi kahawia. Kichwa ni cheupe chenye kinyago. Vidole vyote vina urefu sawa na vina kucha za mviringo bila mfuo kinyume na vipanga na jamaa. Kidole cha nje kinaweza kugeuzwa kuelekea nyuma, kiasi kwamba koho anaweza kushika mawindo kwa vidole viwile mbele na viwili nyuma. Hii inafaa hasa akikamata samaki wenye kuteleza. Koho hula samaki takriban pekee, lakini pengine hukamata wagugunaji, amfibia, watambaazi na ndege wengine. Hutengeneza tago lao kwa vijiti juu ya mti, mhimili ya huduma za umma au mwamba. Jike huyataga mayai 2-4.

Spishi ya Afrika

  • Pandion haliaetus Koho Magharibi (Western Osprey)
    • Pandion h. haliaetus Koho wa Ulaya (Eurasian Osprey)

Spishi za mabara mengine

  • Pandion cristatus (Eastern Osprey)
  • Pandion haliaetus (Western Osprey)
    • Pandion h. carolinensis (American Osprey)
    • Pandion h. haliaetus (Eurasian Osprey)
    • Pandion h. ridgwayi (Caribbean Osprey)

Picha

Marejeo

Tags:

Koho Spishi ya AfrikaKoho Spishi za mabara mengineKoho PichaKoho MarejeoKohoCarolus Linnaeus

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Alama ya barabaraniMadiniChuraAfrika ya MasharikiChris Brown (mwimbaji)SikukuuBustani ya EdeniDioksidi kaboniaRobin WilliamsMadhara ya kuvuta sigaraMwanzoMichelle ObamaMlo kamiliAina za udongoChuo Kikuu cha Dar es SalaamHaitiMekatilili Wa MenzaSumakuUgonjwa wa moyoAntibiotikiJotoUandishiBikiraTungo sentensiUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaHistoria ya KiswahiliUrusiZakaHali maadaBahari ya HindiUkimwiLuis MiquissoneBaraza la mawaziri TanzaniaUkoo27 MachiKondoo (kundinyota)MakkaKiwakilishi nafsiUlayaMfumo wa upumuajiReal BetisHektariMkondo wa umemeMuzikiUsafi wa mazingiraAsiliNgiriChombo cha usafiri kwenye majiMsamiatiChadNgw'anamalundiOrodha ya viongoziLugha ya taifaYoweri Kaguta MuseveniAganoUtafitiMauaji ya kimbari ya RwandaUwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius NyerereUbuyuSemiUbatizoNguvaOrodha ya MiakaJustin BieberNomino za wingiSamaki🡆 More