Mtakatifu Kizito (1872 - Namugongo, Uganda, 3 Juni 1886) ni mmojawapo wa Wafiadini wa Uganda, mdogo kuliko wote.
Alichomwa moto kwa ajili ya imani yake kwa Yesu Kristo akiwa na umri wa miaka 14 tu. Kidogo tu kabla hajauawa alibatizwa na katekista Karolo Lwanga.
Pamoja na wenzake alitangazwa na Papa Benedikto XV kuwa wenye heri tarehe 6 Juni 1920, halafu na Papa Paulo VI kuwa mtakatifu tarehe 18 Oktoba 1964 huko Roma.
Sikukuu yake ni tarehe 3 Juni kila mwaka.
Ni msimamizi wa watoto na wa shule za msingi.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Kizito, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.