Jamhuri Ya Kisovyeti Ya Kijamii Ya Kimoldova

Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kimoldova ilikuwa kati ya jamhuri wanachama 15 za Umoja wa Kisovyeti hadi 1991.

Jina lake liliandikwa kwa Kikirili "Република Советикэ Сочиалистэ Молдовеняскэ (republika sovyetike sotsialiste moldovenyaske) au kwa maandiko ya Kilatini: Republica Sovietică Socialistă Moldovenească; kwa Kirusi: Молдавская Советская Социалистическая Республика.

Jamhuri Ya Kisovyeti Ya Kijamii Ya Kimoldova
Bendera ya Moldova ya Kisovyeti
Jamhuri Ya Kisovyeti Ya Kijamii Ya Kimoldova
Mahali pa Moldova katika Umoja wa Kisovyieti

Iliundwa 1940 kutokana maeneo mawili:

  • a) sehemu ya Jamhuri ya kujitawala ya Kisovyeti ya Kijamii Moldova iliyokuwa sehemu ya Jamhuri ya Kisovyeti ya Ukraine hadi 1940
  • b) eneo la Bessarabia liliowahi kuwa chini ya Urusi hadi 1918 lakini likatwaliwa na Romania baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Mkataba wa Hitler na Stalin wa 1940 ikarudi chini ya Umoja wa Kisovyeti.

Wakazi wa sehemu hii ni hasa Waromania lakini kuna mchanganyiko na Warusi na Waukraine pia.

Wakati wa kuachana kwa Umoja wa Kisovyeti jina likabadilishwa kuwa Jamhuri ya Moldava lililotangaza uhuru wake 27 Agosti 1991 kuwa Moldova.

Tags:

1991KikiriliKilatiniKirusiUmoja wa Kisovyeti

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

UchaguziSimba (kundinyota)Kiambishi tamatiMkoa wa ShinyangaUislamuBiasharaAina za manenoKilimoNgiriKichochoLilithKata za Mkoa wa MorogoroPesaMjombaUandishiWarakaMaudhuiMkoa wa PwaniMpira wa miguuWaziriKupatwa kwa JuaBinadamuMoyoMbuniMisimu (lugha)UzalendoWilaya ya ArushaUmoja wa AfrikaTarafaStadi za maishaMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaManispaaUtamaduniMlongeHisiaAsili ya KiswahiliKisononoVitenzi vishiriki vipungufuMtumbwiAgano JipyaMbeya (mji)ShengMadiniMiundombinuNimoniaMnyoo-matumbo MkubwaOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaHistoria ya KanisaWayback MachineUgandaRisalaFani (fasihi)Mkoa wa RuvumaMkanda wa jeshiWilaya ya IlalaTafsiriNgonjeraUzazi wa mpangoTabianchiPentekosteMagonjwa ya machoAbedi Amani KarumeKonsonantiPapaWangoniMbezi (Ubungo)ImaniHarmonizeNdoaUtendi wa Fumo LiyongoKisimaWahaBlogu🡆 More