Hori Kuu ya Australia ni hori kubwa iliyopo upande wa kusini wa Bara la Australia.
Kuna namna tofauti za kuangalia sehemu hii ya bahari kati ya wataalamu wa Australia na wataalamu wa kimataifa.
Taasisi ya Hidrografia ya Autralia inafafanulia hivi:
Mipaka yake ni Rasi Pasley katika Australia ya Magharibi na Rasi Carnot katika Australia Kusini zilizo na umbali wa km 1,160. Taasisi hii inatazama Hori Kuu ya Australia kuwa sehemu ya Bahari ya Kusini.
Shirika la Kimataifa la Hidrografia linaangalia eneo kubwa zaidi likitazama mstari baina ya Rasi ya Magharibi ya Howe (35°08′S 117°37′E) hadi Rasi ya Kusini Magharibi ya Kisiwa cha Tasmania kuwa mpaka wa kusini. Kwao hori ni sehemu ya Bahari Hindi.
Hakuna miji mikubwa kwenye pwani hiyo. Tabianchi ya pwani ni yabisi, sehemu kubwa ni tambarare inayoitwa "Nullarbor" inayomaanisha "pasipo miti",
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Hori Kuu ya Australia, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.