Dennis Brutus: Mwanaharakati na mwandishi wa Afrika Kusini (1924-2009)

Dennis Brutus (28 Novemba 1924 - 26 Desemba 2009) alikuwa mwandishi wa Afrika Kusini.

Kwa vile aliandika dhidi ya ubaguzi wa rangi alifungwa jela na baadaye kuishi uhamishoni 1966-1990. Hasa alitunga mashairi na alifundisha kama profesa wa ushairi nchini Marekani.

Dennis Brutus: Wasifu [2], Maandishi yake [3][4], Angalia pia
Dennis Brutus (1967)

Wasifu

Dennis Brutus alizaliwa tarehe 28 Novemba, mwaka wa 1924 mjini Salisbury, Rhodesia, ambapo sasa huitwa Harare nchini Zimbabwe. Alisomewa kwenye Paterson High School nchini Afrika Kusini na kupata ushahada wake wa kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Fort Hare katika somo la Kiingereza mwaka wa 1947. Mwaka wa 1950 alimwoa May Jaggers, wakawa na watoto wanane. Kuanzia 1948 hadi 1961, Brutus alifundisha Kiingereza na Kiafrikaans kama mwalimu wa sekondari mjini Port Elizabeth. Mwaka wa 1960 alianza pia kufanya kazi kama mwandishi wa habari. Kwa vile aliandika dhidi ya siasa ya apartheid, alifungwa jela kisiwani mwa Robben kwa miezi 18 (1964-65), na kutoka Afrika Kusini mwaka wa 1966. Uhamishoni kwanza alifanya kazi mjini London kwa shirika la International Defence and Aid Fund. Mwaka wa 1971 akahamia Marekani. Kule akawa profesa wa chuoni, kwanza kwa somo la Kiingereza katika Chuo Kikuu cha Northwestern mjini Evanston (1971-85), na hatimaye tangu mwaka wa 1986 akawa profesa katika idara ya elimu ya kijamii ya watu weusi, Chuo Kikuu cha Pittsburgh.

Maandishi yake

  • Sirens, Knuckles, Boots (mashairi, 1963)
  • Letters to Martha (mashairi, 1968)
  • Poems from Algiers (mashairi, 1970)
  • Thoughts Abroad (mashairi, 1970, aliyoyatolea chini ya jina la John Bruins)
  • A Simple Lust (mashairi, 1973)
  • China Poems (mashairi, 1975)
  • Stubborn Hope (mashairi, 1978)
  • Salutes and Censures (mashairi, 1982)
  • Airs and Tributes (mashairi, 1989)
  • Still the Sirens (mashairi, 1993)
  • Remembering Soweto (mashairi, 2004)
  • Leafdrift (mashairi, 2005)

Angalia pia

Marejeo

Tags:

Dennis Brutus Wasifu [2]Dennis Brutus Maandishi yake [3][4]Dennis Brutus Angalia piaDennis Brutus MarejeoDennis Brutus1924200926 Desemba28 NovembaAfrika KusiniMarekaniUbaguzi wa rangi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

KariakooBibliaWilaya ya KinondoniTawahudiMlima wa MezaOrodha ya kampuni za TanzaniaTanganyika (maana)TabianchiUfugajiMkoa wa KilimanjaroAsidiHerufiHalmashauriMkoa wa MbeyaMoscowKiongoziLigi Kuu Tanzania BaraNamba tasaJamiiUshairiMagharibiMauaji ya kimbari ya RwandaTiktokHaki za watotoBenjamin MkapaKiarabuTungo kishaziEe Mungu Nguvu YetuDiamond PlatnumzMitume wa YesuOrodha ya Marais wa KenyaWaziriTabataInsha ya wasifuOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaMshubiriOrodha ya vyama vya siasa TanzaniaHistoria ya Kanisa KatolikiVasco da GamaUharibifu wa mazingiraBiasharavvjndSteve MweusiMkwawaNyangumiPunda miliaKitenzi kishirikishiMafurikoWilayaVipera vya semiUvimbe wa koromeo usababishwao na streptokokiAunt EzekielMunguWachaggaAfrikaMkoa wa ManyaraPijiniMlongeMatiniOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaMkoa wa DodomaPaul MakondaHurafaTarafaHifadhi ya SerengetiKiimboHomoniBidiiKukiKiumbehaiMadiniArsenal FCSaratani ya mlango wa kizaziMsokoto wa watoto wachangaWanyaturuMsitu🡆 More