Aleksanda Wa Yerusalemu

Aleksanda wa Yerusalemu (Kapadokia, leo nchini Uturuki, karne ya 2 – Kaisarea Baharini, leo nchini Israeli 251 hivi) alikuwa askofu wa Yerusalemu kwa miaka mingi hadi kifodini chake.

Mjini Yerusalemu alianzisha maktaba muhimu na chuo.

Aleksanda Wa Yerusalemu
Picha takatifu ya Mt. Aleksanda wa Yerusalemu.

Tangu kale ametambuliwa kuwa mtakatifu mfiadini na babu wa Kanisa.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 18 Machi au 22 Desemba.

Maisha

Aleksanda alizaliwa katika familia ya Kipagani akapata elimu bora iliyomfanya ajue falsafa na dini mbalimbali hadi akajiunga na Ukristo.

Hapo alikwenda Misri kuhudhuria Chuo cha Kikristo cha Aleksandria akafahamiana na Origen. Huko alifungwa hadi mwaka 211 kutokana na dhuluma ya kaisari Septimius Severus.

Mwaka 212 alifika Yerusalemu akawa askofu mwandamizi wa Narsisi wa Yerusalemu, na baada ya kushika uongozi kamili wa jimbo alishughulikia elimu ya Kikristo kwa kuanzisha shule na maktaba kwa mfano wa Aleksandria. Pia alimtetea Origen na kumpa upadirisho.

Dhuluma mpya za kaisari Decius zilipoanza alifungwa tena na kuteswa hadi kuuawa bila kujali uzee wake hata akafariki kifungoni.

Maandishi yake

Kati ya maandishi yake mengi, zimetufikia sehemu tu za barua nne katika vitabu vya Eusebi wa Kaisarea.

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Aleksanda Wa Yerusalemu  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.

Tags:

Aleksanda Wa Yerusalemu MaishaAleksanda Wa Yerusalemu Maandishi yakeAleksanda Wa Yerusalemu Tazama piaAleksanda Wa Yerusalemu TanbihiAleksanda Wa Yerusalemu Viungo vya njeAleksanda Wa Yerusalemu251AskofuChuoIsraeliKaisarea BahariniKapadokiaKarne ya 2KifodiniMaktabaUturukiYerusalemu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Lahaja za KiswahiliNetiboliOrodha ya watu maarufu wa TanzaniaMisemoMike TysonTarakilishiNevaMkoa wa KigomaIsraelMalawiKrismasiUgonjwa wa uti wa mgongoJumuiya ya MadolaBahari ya HindiTeknolojia ya habariNgamiaKilatiniMlo kamiliMkutano wa Berlin wa 1885Kondoo (kundinyota)Zuhura YunusKitunguuLahajaMeliKataTelevisheniOrodha ya vyama vya kisiasa nchini KenyaJogooMuda sanifu wa duniaUgonjwa wa kuharaNdoa katika UislamuVipera vya semiUhuru wa TanganyikaWapareKiumbehaiDubaiMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaDizasta VinaAbby ChamsKukuFid QAslay Isihaka NassoroAunt EzekielYuda IskariotiMamaMtende (mti)Fani (fasihi)Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifaRitifaaKiunzi cha mifupaShomari KapombeNdegeOrodha ya miji ya MarekaniRwandaUchimbaji wa madini nchini TanzaniaLeopold II wa UbelgijiWazaramoMjasiriamaliMatendeUtegemezi wa dawa za kulevyaMkoa wa MbeyaAsidiKiraiVipaji vya Roho MtakatifuInjili ya MathayoRita wa CasciaZabibuJackie ChanOrodha ya Marais wa TanzaniaBrazilUsawa (hisabati)🡆 More