Aleksanda wa Konstantinopoli (264 hivi - 337 hivi) alikuwa askofu wa Bizanti, baadaye askofu mkuu wa kwanza wa mji huo kwa jina jipya la Konstantinopoli, leo Istanbul nchini Uturuki, kuanzia mwaka 314 hadi kifo chake.
Inasemekana kwanza alikuwa mmonaki kutoka Calabria, Italia Kusini.
Alipinga kwa nguvu zote Uario bila kujali vitisho wa kaisari Konstantino Mkuu na wengineo.
Anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi tangu kale kama mtakatifu.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Aleksanda wa Konstantinopoli, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.