Ufalme wa Yuda (kwa Kiebrania מַמְלֶכֶת יְהוּדָה, Mamlekhet Yehuda) ulikuwa nchi ya Mashariki ya Kati katika karne ya 10 KK hadi karne ya 6 KK.Mara nyingi unaitwa ufalme wa Kusini kwa sababu ulitokana na mgawanyiko wa Ufalme wa Israeli ulioendelea upande wa kaskazini.
Ufalme huo uliongozwa daima na ukoo wa Daudi, isipokuwa miaka 6 (842 KK - 837 KK) aliposhikwa utawala malkia Atalia, binti au dada wa mfalme wa Israeli Ahabu. Hata hivyo kwa muda mrefu watawala wa Yuda walikuwa vibaraka wa Ashuru au nchi nyingine za jirani.).
Hatimaye, chini ya mfalme Sedekia, mfalme Nebukadneza II wa Babuloni aliangamiza ufalme huo na mji mkuu wake, Yerusalemu, mwaka 587, akihamisha kwa awamu tatu wakazi wake hadi Mesopotamia.
Mwaka 539 Koreshi Mkuu, mfalme wa Persia, aliteka Babuloni na kuruhusu Wayahudi warudi kwao, si tena kama ufalme, bali kama wilaya iliyoitwa Yehud, chini ya Zerubabeli, kitukuu wa Yekonia, wa pili kuanzia mwisho kati ya wafalme wa Yuda.
|title=
(help)|title=
(help)|title=
(help)|=
ignored (help)Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yuda (ufalme) kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Yuda (ufalme), which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.