Tel Aviv

Tel Aviv-Yafa (kwa Kiebrania תֵּל־אָבִיב-יָפו; kwa Kiarabu تَلْ أَبِيبْ-يَافَا) ni mji mkubwa wa pili nchini Israel, wenye wakazi 460,613 (2019).

Rundiko la mji kuna watu zaidi ya milioni 3. Mji uko kando ya bahari ya Mediteranea.

Tel Aviv
Uso wa Tel Aviv-Yafa upande wa pwani

Historia

Mji ulitokana na maungano ya miji ya Yafa na Tel Aviv mwaka 1949 baada ya vita ya Kiarabu-Kisraeli ya 1948. Wakati ule Tel Aviv ilikuwa mji mkubwa na Yafa ilibaki na watu wachache tu baada ya kukimbia kwa wakazi Waarabu wengi vitani.

Tel Aviv ilianzishwa kando ya mji wa kale wa Yafa mwaka 1909 na Wayahudi waliohamia Palestina kutoka Ulaya. Mwanzoni ilikuwa kitengo tu cha Yafa kilichojitawala lakini kiliendelea kukua haraka kushinda mji wa kale kikawa manisipaa mwaka 1934.

Wakati wa utawala wa Uingereza Tel Aviv ilikuwa kitovu cha maisha ya Kiyahudi katika Palestina. Hadi leo Tel Aviv-Yafa ni kitovu cha kiutamaduni na cha kiuchumi cha nchi ya Israel.

Marejeo

Viungo vya nje

Tags:

2019BahariIsraelKiarabuKiebraniaMediteraneaMilioniMji

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

MazingiraKisukuruAgano JipyaSumakuUbongoDamuWilaya ya IlalaOrodha ya Makamu wa Rais TanzaniaMohammed Gulam DewjiMkoa wa PwaniUtoaji mimbaFasihiUkristoShengRupiaMkoa wa DodomaMwakaSarufiVita Kuu ya Kwanza ya DuniaKata za Mkoa wa MorogoroUaMeta PlatformsOrodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watuUzazi wa mpangoNyangumiMapenzi ya jinsia mojaAmri KumiLilithNgw'anamalundiKabilaLatitudoUtendi wa Fumo LiyongoDoto Mashaka BitekoFonolojiaRufiji (mto)MwanaumeAzimio la ArushaHaitiEl NinyoNevaOrodha ya makabila ya TanzaniaMajira ya mvuaUtandawaziUzazi wa mpango kwa njia asiliaJose ChameleoneIndonesiaVokaliRushwavvjndInsha ya wasifuOrodha ya vitabu vya BibliaWayahudiVitamini CDar es SalaamVichekeshoKanye WestNuktambiliMamba (mnyama)UgandaRejistaChuo Kikuu cha Dar es SalaamSimu za mikononiTungo kiraiIsimujamiiMafumbo (semi)Kiambishi awaliKamusiSwalaStashahadaMimba za utotoniMr. BlueMwanamkeUNICEF🡆 More