Tatizo La Kutojizuia Kurudiarudia Tendo

Tatizo la kutojizuia kurudiarudia tendo (kwa Kiingereza: obsessive-compulsive disorder, kifupi: OCD) ni tatizo la akili ambapo mtu huhisi haja ya kuangalia vitu mara kwa mara, kufuata utaratibu fulani mara kwa mara, au kuwa na mawazo yaleyale mara kwa mara.

Watu hao hawana uwezo wa kudhibiti ama mawazo au shughuli kwa zaidi ya kipindi kifupi. Shughuli za kawaida ni kama vile kuosha mikono, kuhesabu vitu, na kuangalia iwapo mlango umefungwa. Wengine wanaweza kuwa na ugumu wa kutupa vitu nje. Shughuli hizo hutokea kiasi kwamba maisha ya kila siku yanaathirika vibaya. Hii mara nyingi hutokea zaidi ya saa moja kwa siku.

Watu wazima wengi hugundua kwamba tabia hizo hazina maana. Hali hiyo inahusiana na mitetemo ya neva usoni, tatizo la kuwa na wasiwasi kila mara, na kuongezeka kwa hatari ya kujiua.

Chanzo

Chanzo hakijulikani ila kuna visababishi fulani vya jenetikia, hivyo pacha wanaofanana huathiriwa sana mara nyingi kuliko pacha wasiofanana. Vipengele vya hatari ni kama vile historia ya unyanyasaji wa mtoto au tukio linalosababisha mawazo mazito. Baadhi ya hali zimeshawekwa kwenye kumbukumbu kutokea kwa sababu ya maambukizi. Utambuzi unategemea dalili na huhitaji kuondoa vyanzo vingine vinavyohusiana na dawa au tiba.

Vipimo vya viwango kama vile Yale–Brown Obsessive Compulsive Scale (Y-BOCS) vinaweza kutumika ili kutathmini ukali wake.

Matatizo mengine yaliyo na dalili sawa ni pamoja na tatizo la kuwa na wasiwasi kila mara, tatizo la kuwa na huzuni kali kwa muda mrefu, tatizo la kula isivyo kawaida, tatizo la kuwa na mtetemo wa neva usoni, na tatizo la akili linalomfanya mtu kurudiarudia tabia fulani ya kibinafsi.

Tiba

Matibabu yanajumuisha ushauri, kama vile tiba ya tabia za utambuzi (CBT), na wakati mwingine dawa za kutibu huzuni kama vile kuchagua kizuizi cha ufyonyaji upya wa serotonini (SSRIs) au dawa ya kutibu matatizo ya hofu, wasiwasi na huzuni (clomipramine).

Tiba ya tabia za utambuzi (CBT) kwa tatizo hili (OCD) huhusisha kuongeza kuwekwa wazi kwa chanzo cha shida huku huruhusu tabia ya kujirudia kutotokea. Huku dawa ya kutibu matatizo ya hofu, wasiwasi na huzuni (clomipramine) huonekana kufanya kazi sawa na kuchagua kizuizi cha ufyonyaji upya wa serotonini (SSRIs), ina madhara mengi hivyo huachwa kwanza ili itumike kukihitajika tu. Dawa za kutibu magonjwa ya kisaikolojia zisizo za kawaida zinaweza kuwa muhimu zikitumika pamoja na SSRI katika hali za kukataa matibabu lakini pia zinahusishwa na hatari ya ongezeko la madhara. Bila matibabu, hali hiyo mara nyingi hudumu kwa miongo.

Uenezi

Tatizo hili huathiri karibu 2.3% ya watu kwa wakati fulani maishani mwao. Viwango katika mwaka fulani ni karibu 1.2%, na hutokea kote ulimwenguni. Si kawaida kwa dalili kuanza baada ya umri wa miaka 35, na nusu ya watu huwa na matatizo kabla ya umri wa miaka 20. huku wanaume na wanawake huathiriwa kwa viwango sawa.

Tanbihi

Viungo vya nje

Tatizo La Kutojizuia Kurudiarudia Tendo 
Wiki Commons ina media kuhusu:

Tags:

Tatizo La Kutojizuia Kurudiarudia Tendo ChanzoTatizo La Kutojizuia Kurudiarudia Tendo TibaTatizo La Kutojizuia Kurudiarudia Tendo UeneziTatizo La Kutojizuia Kurudiarudia Tendo TanbihiTatizo La Kutojizuia Kurudiarudia Tendo Viungo vya njeTatizo La Kutojizuia Kurudiarudia TendoKifupiKiingerezaMaishaMlangoVitu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Tanganyika (ziwa)Ligi Kuu Uingereza (EPL)Historia ya KanisaTungoEthiopiaMkutano wa Berlin wa 1885UmememajiOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaNabii EliyaWhatsAppJamhuri ya Watu wa ZanzibarMkoa wa LindiKalenda ya KiislamuNguruwe-kayaSinagogiLughaKaswendeHifadhi ya SerengetiAla ya muzikiAmina ChifupaMamaUkutaMange KimambiLongitudoMwanzo (Biblia)Kiwakilishi nafsiMshubiriJamhuri ya Kidemokrasia ya KongoWameru (Tanzania)Shukuru KawambwaUtendi wa Fumo LiyongoPumuKoloniWimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiSah'lomonMimba kuharibikaKifua kikuuAgostino wa HippoUtoaji mimbaUbaleheTanganyikaKichochoHussein Ali MwinyiWilaya ya IlalaInsha za hojaHadhiraKiolwa cha anganiLeonard MbotelaKukiSaidi NtibazonkizaAKamusi ya Kiswahili sanifuNdiziAsili ya KiswahiliWapareWayback MachineOrodha ya viongoziApril JacksonVitamini CMkuu wa wilayaMuda sanifu wa duniaEe Mungu Nguvu YetuGoba (Ubungo)MtumbwiVivumishiNyukiMbwana SamattaMkoa wa PwaniMlima wa MezaBendera🡆 More