Publius (au Gaius) Cornelius Tacitus (56 hivi - 120 hivi BK) alikuwa mwanasiasa na mwanahistoria wa Dola la Roma.
Vitabu vyake maarufu vilivyotufikia kwa sehemu tu vinaitwa kwa Annales na Historiae. Vinasimulia historia ya dola hilo kuanzia mwaka 14 hadi 70.
Maandishi yake mengine yanahusu ufundi wa kutoa hotuba (Dialogus de oratoribus), Ujerumani (De origine et situ Germanorum), na maisha ya mkwe wake, jenerali Gnaeus Julius Agricola, aliyeteka sehemu kubwa ya Britania (De vita et moribus Iulii Agricolae).
Tacitus anahesabiwa kati ya wanahistoria bora wa Roma ya Kale.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Tacitus kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Tacitus, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.