Saturnus

Saturnus ni jina la mungu mmojawapo aliyeabudiwa katika Roma ya Kale.

Aliaminiwa kuwa mungu aliyehusika mambo ya kilimo na mavuno. Alitolewa sadaka kwa ajili ya kustawi kwa mazao.

Saturnus
Sanamu hii ya Saturnus imepatikana katika Tunisia yaonyeshwa katika makumbusho ya Bardo

Waroma wa Kale walitumia kuhusu Saturnus masimulizi waliopokea kutoka kwa Wagiriki ilhali walimwona kama jina mbadala kwa mungu wa Kigiriki Kronos; huyu alikuwa mwana wa mungu wa mbingu Urano na mungu wa kike wa ardhi Gaia. Alimpindua babake kwa kukata uume wake. Baadaye alihofia ya kwamba watoto wake watampindua vile hivyo alikula watoto wake wote isipokuwa mwana wa sita Jupiter alifichwa mbele yake. Saturnus alipaswa kukimbia akafikia Italia alipowafundisha wenyeji elimu ya kilimo.

Sikukuu ya Saturnus iliitwa "Saturnalia" ni siku kadhaa kuanzia 17 Desemba zilizokuwa sherehe kubwa huko Roma.

Alama yake angani ilikuwa sayari ya sita yaani Zohali inayoitwa hadi leo kwa jina la "Saturn" katika lugha za Ulaya.

Siku ya Jumamosi huitwa "siku ya Saturnus" yaani Saturday hadi leo kwa Kiingereza na Kiholanzi.

Tags:

Roma ya Kale

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

WasukumaArsenal FCNguruwe-kayaJinsiaMohammed Gulam DewjiVidonda vya tumboBaraVielezi vya idadiNgiriPasifikiNomino za jumlaUnyagoWaziriCleopa David MsuyaSumakuSensaKaswendeDivaiKata za Mkoa wa Dar es SalaamJumuiya ya Afrika MasharikiKondomu ya kikeTamathali za semiLatitudoUzalendoEthiopiaMlongeWarakaKuki25 ApriliBongo FlavaPijiniTenzi tatu za kaleUtendi wa Fumo LiyongoUkoloniWaheheUzazi wa mpangoUfugaji wa kukuMahakama ya TanzaniaSimu za mikononiLigi Kuu Tanzania BaraBahari ya HindiMkoa wa Dar es SalaamMkoa wa SingidaYesuShahawaKanga (ndege)Manchester CityMuungano wa Tanganyika na ZanzibarOrodha ya nchi kufuatana na wakaziHistoria ya KanisaUgonjwa wa kuharaMunguKiarabuKipindupinduOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaMkoa wa MorogoroIsraelMkoa wa TaboraMasafa ya mawimbiMkoa wa PwaniUchaguziMaktabaBunge la TanzaniaChristopher MtikilaRupiaViwakilishi vya pekeeSimba (kundinyota)Tungo sentensiVita ya Maji MajiSiriPaul MakondaMahindiPunda miliaPombeGeorDavie🡆 More