Kunegunda wa Luxembourg, OSB (975 hivi – Kaufungen, 3 Machi 1040) alikuwa mke wa kaisari wa Dola Takatifu la Kiroma (Ujerumani) Henri II.
Inasemekana waliishi bila kufanya tendo la ndoa na waligawa mali nyingi kwa watu fukara na kufadhili Kanisa kwa namna mbalimbali.
Mwaka mmoja baada ya kufiwa mume wake, aliingia monasterini na kumfanya Kristo kuwa urithi wake kama alivyotamani tangu ujanani.
Alipofariki yeye pia, alizikwa kwa heshima zote karibu na mumewe.
Tarehe 29 Machi 1200 alitangazwa na Papa Innocent III kuwa mtakatifu, kama mumewe.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Machi.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Kunegunda wa Luxemburg, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.