Kilwa Kisiwani

Kwa matumizi mengine ya jina hili tazama Kilwa


Kilwa Kisiwani
Nchi Tanzania
Mkoa Lindi
Wilaya
Kilwa Kisiwani
Msikiti mkuu Kilwa Kisiwani
Kilwa Kisiwani
Boma la Kireno kwenye bandari ya Kilwa Kisiwani

Kilwa Kisiwani ni jina la kijiji kikubwa kwenye Kisiwa cha Kilwa karibu na mji wa Kilwa Masoko katika Mkoa wa Lindi, Tanzania.

Ndipo mahali pa mji wa Kilwa ya kihistoria iliyokuwa mji mkubwa kabisa kati ya miji ya Waswahili katika pwani ya Afrika ya Mashariki wakati wa karne ya 14 hadi karne ya 16 BK.

Mji muhimu zaidi wa Uswahilini

Kuanzia karne ya 11 Kilwa ilikuwa kituo muhimu cha biashara. Kuanzia karne ya 13 na 14 Kilwa ikawa muhimu kuliko Mombasa. Biashara yake ilikuwa dhahabu kutoka Dola la Mwene Mtapa (Zimbabwe), pembe za ndovu, chuma, nazi pamoja na kununua bidhaa kutoka Bara Hindi na Uchina. Sarafu ya dhahabu kutoka Kilwa imepatikana huko Zimbabwe Kuu.

Katika karne ya 14 - kati ya 1330 na 1340 BK - mji ulitembelewa na msafiri Mwarabu Ibn Battuta aliyeacha taarifa ya kwanza ya kimaandishi kuhusu mji huo.

Majengo makubwa yalijengwa yakiwa magofu yao yamesimama hadi leo kama vile msikiti mkuu, Jumba ya kifalme ya Husuni Kubwa, Boma la Kireno Kilwa na mengine mengi.

Kuja kwa Wareno

Kuja kwa Wareno katika karne ya 16 ilivuruga biashara ya Waswahili. Kilwa ikarudi nyuma. Katika karne ya 18 na ya 19 ikapata upya nguvu ya kiuchumi kutokana na biashara ya watumwa. Mwisho wa biashara hiyo ulimaliza utajiri wa Kilwa.

Kilwa leo

Kilwa Kisiwani 
Mojawapo ya majengo ya kale huko Kilwa visiwani

Leo hii Kilwa Kisiwani ipo katika eneo la Tanzania lisilotembelewa kwa urahisi.

Hata hivyo kisiwa ni kati ya Hifadhi za Kiutamaduni muhimu sana za Tanzania, hata imeandikishwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia" (World Heritage).

Katika wilaya hiyo kuna mahali pengine pa urithi wa dunia, Selous.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

  •  . Volume 1: History and archaeology; Volume 2: The finds.
  •  . First published in 1986, ISBN 0-520-05771-6.
  • João de Barros (1552) Décadas da Ásia: Dos feitos, que os Portuguezes fizeram no descubrimento, e conquista, dos mares, e terras do Oriente., Dec. I, Lib. 8, Cap. 6 (p. 223ff)
  • Strong, S. Arthur (1895) "The History of Kilwa, edited from an Arabic MS", Journal of the Royal Asiatic Society, January (No volume number), pp. 385–431. online

Viungo vya nje

Kilwa Kisiwani  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Lindi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kilwa Kisiwani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.

Tags:

Kilwa Kisiwani Mji muhimu zaidi wa UswahiliniKilwa Kisiwani Kuja kwa WarenoKilwa Kisiwani Kilwa leoKilwa Kisiwani Tazama piaKilwa Kisiwani TanbihiKilwa Kisiwani MarejeoKilwa Kisiwani Viungo vya njeKilwa KisiwaniKilwa

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

MamaUongoziKisimaBibliaWabunge wa Tanzania 2020Kitenzi kikuu kisaidiziWajitaNgonjeraMauaji ya kimbari ya RwandaUtumwaMapenziMkoa wa SimiyuDaudi (Biblia)MazingiraKiimboKunguruMfumo wa JuaIsimuUKUTAKigoma-UjijiJamiiGeorDavieMkoa wa LindiUandishiAli Hassan MwinyiMajira ya mvuaNyaniMahakama ya TanzaniaNgano (hadithi)Bahari ya HindiNyukiOrodha ya miji ya TanzaniaOrodha ya Watakatifu WakristoUenezi wa KiswahiliVisakaleNomino za jumlaOrodha ya kampuni za TanzaniaDiglosiaHekalu la YerusalemuJay MelodyPichaUlumbiKoloniKishazi huruBendera ya KenyaSwalaKiwakilishi nafsiNomino za kawaidaJichoMchwaJoyce Lazaro NdalichakoMadawa ya kulevyaJeshi la Ulinzi la Wananchi wa TanzaniaOrodha ya makabila ya KenyaInsha ya wasifuMkoa wa KataviKisaweKomaSumakuRaiaFananiIdi AminKenyaKimara (Ubungo)Ukoloni🡆 More