John von Neumann (28 Desemba 1903 - 8 Februari 1957) alikuwa mtaalamu wa hisabati nchini Marekani.
Alizaliwa Budapest kama mtoto wa familia ya Wahungaria wa Kiyahudi aliyeonekana mapema kuwa na akili bora. Baada ya kumaliza shule alisoma uhandisi Berlin na Zürich akaendelea na msomo ya hisabati. Tangu 1926 alikuwa mwalimu na baadaye proofesa wa hisabati kwenye vyuo vikuu vya Berlin na Hamburg. 1930 alihamia Marekani alipokuwa profesa kwenye chuo kikuu cha Princeton.
John von Neumann | |
---|---|
| |
Alizaliwa | 28 Desemba 1903 Budapest |
Alikufa | 8 Februari 1957 Washington, D.C. |
Nchi | Marekani |
Kazi yake | Mtaalamu wa hisabati |
Anahesabiwa kati ya wanahisabati muhimu zaidi ya karne ya 20. Hisabati yake yalisaidia kuelewa fizikia ya kwanta na kwa hiyo alishiriki katika kazi za kuanzisha bomu ya nyuklia wakati wa vita kuu ya pili ya dunia.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article John von Neumann, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.