Iridi

Iridi ni elementi haba na metali adimu yenye namba atomia 77 katika jedwali la elementi. Alama yake ni Ir. Inahesabiwa katika kundi la Platini. Kati ya metali zote inaathiriwa kidogo kabisa na mmenyuko wa kikemia.

Iridi (iridium)
Iridi
Jina la Elementi Iridi (iridium)
Alama Ir
Namba atomia 77
Uzani atomia 192,217
Ugumu (Mohs) 6.5
Kiwango cha kuyeyuka 2739 K (2466 °C)
Kiwango cha kuchemka 4701 K (4428°C)
Asilimia za ganda la dunia 1·10-7 %

Iridi ilitambuliwa na Smithson Trennant mwaka 1803 pamoja na metali ya Osmi. Alijaribu kuyeyusha madini ya platini katika asidi akakuta metali hizo mbili. Alichagua jina la "iridium" kutokana na neno la Kigiriki "iridios" kwa sababu ya rangi nyingi za chumvi zake. Tabia ya kutomeyuka kulisababisha uteuzi wa iridi kwa aloi ya mita asilia.

Iridi ni kati ya metali haba kabisa duniani. Hutokea pamoja na platini au kama madini ya mchanganyiko pamoja na Osmi. Nchi zenye akiba za Iridi ni hasa Afrika Kusini, Urusi (milima ya Ural), Amerika ya Kaskazini na ya Kusini, Japani, Borneo na Tasmania.

Hutumiwa ndani ya aloi za metali ikiongeza ugumu wa aloi hizo. Mwaka 2007 kilogramu 3,700 za iridi zilitumiwa duniani; kati ya hizo takriban kilogramu 780 ziliingia katika vifaa vya umeme kama plagi za cheche kwenye injini za mwako ndani; 1,100 kg zikatumiwa kwa elektrodi.

Tanbihi

Viungo vya nje

Iridi 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:

Iridi  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Iridi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Kitenzi kishirikishiViwakilishi vya kuoneshaFran BentleyWaluoMnyoo-matumbo MkubwaMnazi (mti)Mkoa wa KageraUfahamuSaidi Salim BakhresaMalengo ya Kiswahili kuwa lugha ya taifaVieleziMajira ya mvuaBarua rasmiHekalu la YerusalemuMtoni (Temeke)Paul MakondaChristopher MtikilaTaswira katika fasihiNjia ya MachoziIfakaraMajeshi ya Ulinzi ya KenyaWahaKomaKaswendeTungo sentensiShetaniTabianchiRose MhandoJohn Raphael BoccoMaigizoMtoto wa jichoUnyenyekevuNgonjeraDiraOrodha ya Magavana wa TanganyikaMfumo wa mzunguko wa damuDhanaSteve MweusiJumapiliKiswahiliMobutu Sese SekoFutiOrodha ya Marais wa MarekaniUmoja wa KisovyetiUrusiUbongoPonografiaKaterina wa SienaMaradhi ya zinaaMpira wa miguuHuduma ya kwanzaTanzaniaWanyama wa nyumbaniNguzo tano za UislamuWairaqwUjasiriamaliNomino za dhahaniaShikamooWasukumaDodoma (mji)EthiopiaMkunduKenyaUhifadhi wa fasihi simuliziUingerezaMapambano ya uhuru TanganyikaViwakilishiMuungano wa Madola ya Afrikaec4tgMsumbijiKitenzi kikuu kisaidiziOrodha ya Marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoSokwe (Hominidae)🡆 More