Fungo

Fungo, fungo wa Afrika, ngawa au paka-zabadi wa Afrika (Civettictis civetta) ni mnyama mbua na spishi pekee ya jenasi yake.

Fungo
Fungo (Civettictis civetta)
Fungo (Civettictis civetta)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Feliformia (Wanyama kama paka)
Familia: Viverridae (Wanyama walio na mnasaba na paka-zabadi)
Nusufamilia: Viverrinae (Wanyama wanaofanana na paka-zabadi)
J.E. Gray, 1821
Jenasi: Civettictis
Pocock, 1915
Spishi: C. civetta
(Schreber, 1776)
Msambao wa fungo
Msambao wa fungo

Pia ni mwanafamilia mkubwa kabisa wa Viverridae. Binturongi ni mfupi lakini mzito kuliko fungo. Spishi hii inatokea mahali pengi pa Afrika kusini kwa Sahara. Hukiakia usiku hasa na kulala mchana katika uoto mzito. Usiku huonekana katika maeneo mbalimbali kutoka msitu mzito hadi mbuga.

Fungo ni mamalia wapweke wenye rangi nyeusi na nyeupe kwa milia na mabaka. Kwa hivyo wanyama hawa ni ngumu kuona vizuri kwa mwanga mhafifu. Wanaweza kutofautishwa pia kwa matako yao makubwa na manyoya ya mgongo yanayoweza kuwekwa wima. Hula vitu vyingi kama wanyama wadogo, wadudu, mayai, mizoga na mimea. Wanaweza kula wadudu na wanyama wenye sumu, kama tandu, majongoo na nyoka. Hugundua mawindo yao kwa harufu na sauti badala ya kuona.

Kama wanyama wengine wa familia yao fungo watoa kioevu kiitwacho civetone au zabadi. Kioevu hiki kipakazwa juu ya miti, mawe n.k. ili kudai eneo lao. Zabadi hutumika katika viwanda vya manukato pia na inavunwa kutoka fungo wafugwao k.m. huko Uhabeshi.

Picha

Marejeo

Tags:

AfrikaJenasiMbugaMnyamaMsituSaharaSpishiViverridae

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Orodha ya majimbo ya MarekaniVivumishi vya sifaAngahewaTovutiRitifaaOrodha ya milima mirefu dunianiKilimoAfrikaHistoria ya KiswahiliMamba (mnyama)TanganyikaSaratani ya mlango wa kizaziHarmonizeShirikisho la Afrika MasharikiMbeya (mji)Vidonge vya majiraClatous ChamaKiunguliaUchawiTashihisiAsili ya KiswahiliJuxChatuNelson MandelaUpepoSayariShinaMaishaMamaKipindi cha PasakaBurundiUandishi wa ripotiMgawanyo wa AfrikaMamlaka ya Mapato ya TanzaniaAli KibaLigi Kuu Uingereza (EPL)Jumapili ya matawiWabena (Tanzania)ItikadiSkautiIsraeli ya KaleAzimio la kaziCristiano RonaldoBoris JohnsonKahawiaMafuta ya wakatekumeniOsimosisiJulius NyerereRwandaTungoJuma kuuUtafitiPasaka ya KiyahudiDNALuis MiquissoneSarufiWasafwaFonimuSemiAdhuhuriHifadhi ya mazingiraKata za Mkoa wa Dar es SalaamMkoa wa ArushaMkoa wa KigomaNguzo tano za UislamuKonsonantiChris Brown (mwimbaji)ItaliaMakkaPasaka ya KikristoSerikaliOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoMmeaUkooMkwawa27 Machi🡆 More