Bunduki ni silaha inayorusha risasi dhidi ya shabaha yake.
Ndani ya bunduki inatokea mlipuko wa baruti na gesi joto za mlipuko zinasukuma risasi kufuata mwelekeo wa kasiba yake. Kutokana na sifa hii huitwa pia silaha ya moto. Kasiba ya bunduki za kisasa huwa na mifuo ndani yake inayosababisha risasi kuzunguka; inaendelea kuzunguka baada ya kutoka nje ya kasiba na mwendo huu unatunza mwelekeo wake. Kipenyo cha risasi ni sawa na kipenyo cha ndani cha kasiba hivyo risasi inagusa kasiba wakati wa kufyatuliwa.
Bunduki ya kisasa huwa na akiba ya ramia katika chemba yake isipokuwa silaha kadhaa za kuwinda. Silaha za kijeshi huwa na chemba zonazoshika risasi zaidi ya 100.
Kwa kawaida neno "bunduki" linataja silaha za moto zenye kasiba ndefu zinazoshikwa mikononi.
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Bunduki, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.