Bishkek (Bichkiek) ni mji mkuu wa Kirgizia.
Ina wakazi 900,000 (2005).
Jiji la Bishkek | |
Nchi | Kirgizia |
---|
Mji ulianzishwa kama kituo cha misafara kwenye barabara ya hariri kati ya China na Mashariki ya Kati. Khan wa Kokand alitengeneza hapa boma lililotwaliwa na jeshi la Urusi 1862 wakati wa uenezaji wa Urusi katika Asia ya Kati.
1878 Warusi walijenga mahali palepale kituo cha kijeshi kwa jina la "Pishpek" (Пишпек). Kituo kikakua haraka kuwa mji kwa sababu wakulima Warusi walipewa mashamba katika eneo hili.
Baada ya mapinduzi ya Urusi ya 1917 mji ulibadilishwa jina ukaitwa "Frunze" (Frunzie) kwa heshima ya jemadari mkomunisti Mikhail Frunze.
Tangu kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti mwaka 1991 mji ukawa mji mkuu wa nchi mpya ya Kirgizia ikarudishwa jina la kale kwa umbo la "Bishkek".
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Bishkek kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Bishkek, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.