Zumari (kutoka jina la Kiarabu; kwa Kiingereza flute) ni ala ya muziki inayopigwa kwa kupulizwa mdomoni.
Umbo lake ni kama bomba jembamba upande wa mdomoni na pana upande unaotokea sauti.
Inapatikana kote duniani. Hewa inapulizwa ndani kwa mdomo kupitia shimo; mkondo wa hewa unapita kwenye kona kali ambako unaanza kutingatinga ukisababisha nguzo ya hewa iliyopo ndani ya bomba kutingatinga pia; mitetemo hii ni sauti.
Urefu wa bomba unafanya tabia ya sauti; kama ni fupi linatoa sauti ya juu; kama ni refu lina sauti ya chini.
Zumari nyingi huwa na mashimo kanda yanayofunikwa na kufunguliwa kwa vidole. Kwa kufungua shimo mchezaji anafupisha au kurefusha nguzo ya hewa ndani ya zumari inayotingatinga na kubadilisha sauti hivyo.
Kuna muundo kadhaa:
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Zumari kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Zumari, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.