Wahiti walikuwa wakazi wa Anatolia (leo nchini Uturuki) ambao mwaka 1600 KK hivi walianzisha dola lenye makao makuu huko Hattusa.
Dola lilifikia kilele cha ustawi wake katikati ya karne ya 14 KK walipotawala sehemu kubwa ya Uturuki wa leo pamoja na Siria, Lebanoni na Iraq kaskazini.
Kijeshi walifaidika sana na matumizi ya magari ya vita ya kukokotwa na farasi.
Baada ya mwaka 1180 KK hivi dola lilisambaratika.
Lugha yao ilikuwa mojawapo ya lugha za Kihindi-Kiulaya.
Katika Biblia wanazungumziwa mara kadhaa wakiwa na uhusiano mwema na Waisraeli.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wahiti kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Wahiti, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.