Mradi Wa Umoja Wa Mataifa Kuhusu Mazingira: Shirika la Umoja wa Mataifa

Mradi wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Mazingira (kifupi: UNEP) ni mojawapo ya mashirika ya UM yaliyo chini ya madaraka ya Baraza la Kiuchumi na Kijamii, yaani ECOSOC .

Mradi Wa Umoja Wa Mataifa Kuhusu Mazingira: Historia, Mkurugenzi wa UNEP, Tanbihi
Bendera ya UNEP.

Mradi huo una kazi ya kuanzisha na kuendeleza miradi ya kuhifadhi mazingira ya binadamu jinsi yalivyo na hatimaye kuyaboresha. Kwa kufanya hivi, UNEP inaonelea kuwa sote tuna jukumu la kuhifadhi na kuboresha mazingira kwa vizazi vijavyo.

Makao makuu yako mjini Nairobi, Kenya.

Historia

UNEP ilianzishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 15 Desemba 1972 kupitia sheria ya ishirini na saba.

Mkurugenzi wa UNEP

Mkurugenzi wa UNEP anajulikana kama mkurugenzi-tekelezi (Executive Director).

Mnamo Disemba 1972 Mkanada Maurice Strong alichaguliwa mkurugenzi tekelezi wa kwanza wa UNEP hadi 1975. Mwandamizi wake alikuwa Mostafa Kamal Tolba kutoka Misri aliyeshika nafasi kwa miaka 17 hadi 1992.

Chini ya hao wakurugenzi umuhimu wa masuala ya mazingira ulianza kueleweka katika nchi nyingi, hasa baada ya mafanikio ya mapatano ya Montreal ya 1987 kuhusu hifadhi ya tabaka la ozoni kwenye angahewa.

Alifuatwa na Elizabeth Dowdeswell (1992–1998), Klaus Töpfer (1998–2006), Achim Steiner (2006–2016), Erik Solheim (2016-2018), Joyce Msuya (2018-2019) na Inger Andersen (2019–sasa).

Tangu mwaka 2018 kaimu mkurugenzi tekelezi ni Mtanzania Joyce Msuya.

UNEP imejihusisha na mpango wa Kyoto kupunguza gesi zinazoongeza joto duniani.

Tanbihi

Viungo vya nje

Tags:

Mradi Wa Umoja Wa Mataifa Kuhusu Mazingira HistoriaMradi Wa Umoja Wa Mataifa Kuhusu Mazingira Mkurugenzi wa UNEPMradi Wa Umoja Wa Mataifa Kuhusu Mazingira TanbihiMradi Wa Umoja Wa Mataifa Kuhusu Mazingira Viungo vya njeMradi Wa Umoja Wa Mataifa Kuhusu MazingiraECOSOCKifupiUM

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

MilanoUtumwaTungo sentensiHistoria ya IranKitenzi kikuu kisaidiziIkwetaSamakiMazungumzoHisiaOrodha ya miji ya TanzaniaMiundombinuNgw'anamalundiUtamaduniMbuga za Taifa la TanzaniaInstagramHistoria ya KanisaTendo la ndoaWilaya za TanzaniaMshororoSarufiUtandawaziUaFisiKutoa taka za mwiliLakabuAlama ya uakifishajiMasharikiMsamahaBenderaMaumivu ya kiunoSensaEe Mungu Nguvu YetuAntibiotikiMajira ya mvuaRupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniAMvuaKisimaMadawa ya kulevyaWagogoWahaSentensiSanaaTungo kiraiMimba za utotoniAlama ya barabaraniKiumbehaiMkoa wa PwaniMichael JacksonOrodha ya Marais wa ZanzibarZiwa ViktoriaWameru (Tanzania)WaziriMeno ya plastikiUajemiOrodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifaDawatiSitiariLongitudoOrodha ya Marais wa MarekaniHadithiUhakiki wa fasihi simuliziUkristoNuktambiliNamba tasaMbezi (Ubungo)KanisaUsanifu wa ndaniOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaMtume PetroJoseph ButikuMajiUkristo barani Afrika🡆 More