Kroisos

Kroisos (kwa Kigir.

Lydia ilikuwa nchi ya Ugiriki ya Kale kwenye maeneo ya magharibi ya Asia Ndogo yaani Uturuki ya leo.

Kroisos
Picha kwenye chungu cha kale inamwonesha Kroisos kwenye kuni atakapoendelea kuchomwa kufuatana na mapokeo ya Herodoti.

Kroisos alikuwa maarufu kwa utajiri wake mkubwa. Chanzo cha utajiri wake kilikuwa dhahabu iliyochimbwa katika milki yake pamoja na kodi ya miji ya biashara na malipo ya miji ya Kigiriki iliyoshindwa naye kwa vita. Waandishi Herodoti na Pausanias walitaja kwamba zawadi zake zilitunzwa kwenye hekalu la Delphi.

Kroisos
Mipaka ya Lydia chini ya Mfalme Kroisos
Kroisos
Sarafu ya dhahabu ya Kroisos, Lydia, mnamo 550 KK.

Croesus anasifiwa kwa kutoa sarafu za kwanza za dhahabu zilizosanifishwa kwa usafi sanifu na uzito maalumu kama pesa rasmi.

Katika tamaduni za Kigiriki na Kiajemi jina la Kroisos likawa kisawe cha mtu tajiri. Kwa lugha za Ulaya kama Kiingereza, semi kama vile "tajiri kama Croesus" au "tajiri kuliko Croesus" hutumiwa hadi leo kuonyesha utajiri mkubwa.

Wakati wa utawala wake milki ya Uajemi chini ya mfalme Koreshi II ilipanusha mipaka yake ndani ya Asia Ndogo na Kroisos aliona hatari kwa utawala wake. Hivyo aliamua kutumia utajiri wake kuajiri jeshi la mamluki na kushambulia Waajemi. Kabla ya kuvuka mto Hadys uliokuwa mpaka wa milki, alituma wajumbe kwa Pythia wa Delfi aliyekuwa mwaguzi mashuhuri katika Ugiriki ya Kale na kutafuta utabiri kuhusu vita aliyopanga. Jibu la Pythia lilikuwa "Ukivuka mto Hadys utaharibu milki kubwa", alilopokea kama utabiri wa ushindi wake. Lakini alishindwa katika vita na Koreshi II na milki iliyoharibika ilikuwa milki yake mwenyewe.

Hatima ya Croesus baada ya ushindi wa Waajemi dhidi ya Lydia haijulikani: Herodoti pamoja na waandishi wengine waliandika kwamba ama Kroisos alijaribu kujiua, au kwamba alihukumiwa na kuchomwa na Waajemi akiwa hai. Wengine waliandika kwamba aliendelea kuishi na kuwa mshauri wa mshindi Koreshi. Xenofoni alidai pia kwamba Koreshi alimweka Kroisos kama mshauri wake, ilhali mwandishi mwingine wa kale aliandika kwamba Koreshi alimteua kuwa gavana wa eneo huko Umedi.

Baada ya kumshinda Kroisos, Koreshi aliiga matumizi ya dhahabu kama sarafu kuu ya ufalme wa Uajemi.

Marejeo

Viungo vya nje

Tags:

547 KK585 KKAsia NdogoKigir.Kilat.Koreshi MkuuMagharibiMfalmeMwakaUajemi ya KaleUgiriki ya KaleUturuki

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Kishazi tegemeziUandishi wa ripotiVieleziKoloniSensaMapinduzi ya ZanzibarJinsiaMilango ya fahamuMzabibuMoscowUpendoBiolojiaWaluguruMsokoto wa watoto wachangaIfakaraNyotaOrodha ya viongoziMaumivu ya kiunoUjerumaniAbrahamuKiambishiMchwavvjndNamba tasaKiongoziMzeituniManispaaBikira MariaNembo ya TanzaniaMajina ya Yesu katika Agano JipyaIndonesiaJumuiya ya MadolaNevaAlizetiWaziriMwana FAKiazi cha kizunguStephane Aziz KiLongitudoDiamond PlatnumzJamhuri ya Watu wa ZanzibarUlimwenguRohoMfumo wa mzunguko wa damuDivaiAla ya muzikiNandyRaiaHarmonizeCleopa David MsuyaKigoma-UjijiBaruaKhalifaUwanja wa Taifa (Tanzania)SiasaVidonge vya majiraMeta PlatformsMtaalaMaradhi ya zinaaUgonjwa wa kuharaHistoria ya IranNyaniAgano JipyaPamboSimu za mikononiFalsafaMkoa wa RukwaYouTubeNimoniaTaswira katika fasihiMeno ya plastiki🡆 More