Kitabu Cha Wamakabayo I

Kitabu cha kwanza cha Wamakabayo ni kimojawapo kati ya vitabu vya deuterokanoni vya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Kitabu Cha Wamakabayo I
Matathia akimuua Myahudi mwasi, mchoro wa Philippe De Loutherbourg.

Kinasimulia jinsi Wayahudi, wakiongozwa na familia ya Wamakabayo, walivyopambana kwanza na mfalme Antioko IV (aliyejiita Antioko Epifane) halafu na Wayunani wengine katika karne ya 2 KK (175-135 KK).

Kitabu hiki si mbali na matukio kinayoyasimulia, kwa kuwa kiliandikwa kati ya mwaka 140 KK na 130 KK kwa lugha ya Kiebrania, ingawa katika lugha hiyo asili hatuna nakala yoyote, bali tuna tafsiri ya Kigiriki tu katika Septuaginta.

Mwandishi wake hajulikani, lakini kitabu hiki kinaonyesha alikuwa Myahudi wa Palestina, alipenda taifa na dini yake ya Uyahudi, na alijua kwa dhati masuala ya teolojia.

Mfalme huyo alijaribu kulazimisha Wayahudi kufuata utamaduni na dini ya Kiyunani, jambo ambalo lilipingwa na waamini waadilifu wakiongozwa na Matathia na wanae Yuda Mmakabayo, Yonathani Mmakabayo na Simoni Mmakabayo.

Tofauti na kitabu cha Tobiti, kitabu cha Yudith na Kitabu cha Esta, kitabu hiki kinajitahidi kusimulia taratibu za habari za historia, ingawa kinasifu ushujaa wa Wayahudi.

Mwandishi hamtaji Mungu, isipokuwa kwa kusema "mbingu"; lakini wapigania uhuru wanategemea sala. Hivyo hatimaye ushindi uliopatikana unahesabiwa ni tunda la msaada wa Mungu.

Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Marejeo

  • Bartlett, John R. 1998. 1 Maccabees. Sheffield, UK: Sheffield Academic Press.
  • Borchardt, Francis. 2014. The Torah in 1 Maccabees: A Literary Critical Approach to the Text. Boston: Walter de Gruyter.
  • Goldstein, Jonathan A. 1976. I Maccabees: A New Translation, with Introduction and Commentary. Anchor Bible 41. Garden City, NY: Doubleday.
  • Lanzinger, Daniel. 2015. "Alcimus’ Last Command: History and Propaganda in 1 Maccabees 9:54." Journal for the Study of Judaism 46, no. 1: 86–102.
  • Williams, David S. 1999. The Structure of 1 Maccabees. Washington, DC: Catholic Biblical Association.

Viungo vya nje

Kitabu Cha Wamakabayo I 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:


Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki

Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

Kitabu Cha Wamakabayo I  Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitabu cha Wamakabayo I kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Agano la KaleBiblia ya KikristoDeuterokanoniVitabu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Kifua kikuuEthiopiaHoma ya matumboMuunganoUongoziChatuMazingiraDemokrasiaMmeaHerufiNdiziLigi Kuu Uingereza (EPL)MachweoNgiriMmeng'enyoUzazi wa mpango kwa njia asiliaTungo sentensiAmri KumiUtumbo mwembambaKiswahiliDar es SalaamUchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020Vivumishi vya urejeshiUhifadhi wa fasihi simuliziUpendoUkongaMazungumzoUchawiSoko la watumwaMabiboOrodha ya kampuni za TanzaniaKataZabibuMaigizoKata za Mkoa wa Dar es SalaamSadakaEe Mungu Nguvu YetuMkoa wa SongweHekalu la YerusalemuMkoa wa RukwaDodoma MakuluEdward SokoineMbadili jinsiaUfisadiWanyaturuMaziwa ya mamaJumuiya ya Afrika MasharikiKhadija KopaNomino za pekeeHistoria ya TanzaniaSheriaKamusiMuhammadImani24 ApriliSaidi NtibazonkizaUgonjwa wa uti wa mgongoMkutano wa Berlin wa 1885BungeDoto Mashaka BitekoOrodha ya Marais wa TanzaniaMaudhuiMkataba wa Helgoland-ZanzibarBendera ya TanzaniaTungo kishaziSimba S.C.TiktokRitifaaSayansiOrodha ya milima mirefu dunianiUmeme🡆 More