Jimbo la Mataifa ya Kusini (kwa Kiamhari: ደቡብ ብሔሮች ብሔረሰቦችና ሕዝቦች, Ye-Debub Bəheročč Bəheresebočč-ənna Həzbočč; kwa Kiingereza Southern Nations, Nationalities, and Peoples’ Region, kifupi: SNNPR) ni moja kati ya majimbo 12 ya kujitawala ya Ethiopia.
Jimbo liko kusini mwa nchi, likipakana na Kenya upande wa kusini, Sudan Kusini upande wa magharibi na majimbo ya Ethiopia ya Gambela upande wa kaskazini na Oromia upande wa kaskazini, mashariki na kusini-mashariki.
Tofauti na majimbo mengine ya Ethiopia yenye kabila au kundi 1 hasa, hapa kuna vikundi vingi vidogovidogo kwa jumla 45. Wakazi wengi huishi mashambani ama vijijini au kama wahamiaji katika makambi yao ya kuhama.
Mji mkuu wa jimbo ni Awassa, lakini baada ya jimbo kumegwa, mji huo umekuwa wa jimbo la Sidama, hivyo unafikiriwa mwingine.
Addis Abeba | Afar | Amhara | Benishangul-Gumuz | Dire Dawa | Gambela | Harar | Oromia | Sidama | Somali | Mataifa ya Kusini | Tigray |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Jimbo la Mataifa ya Kusini, Ethiopia, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.