Hutu Junubi (kwa Kilatini na Kiingereza Piscis Austrinus) ni jina la kundinyota ndogo kwenye angakusi ya Dunia yetu.
Ni tofauti na kundinyota Hutu (au Samaki, Piscis).
Hutu Junubi (Piscis Austrinus) lipo karibu na ikweta ya anga linapakana na makundinyota jirani ya Mbuzi (pia Jadi au lat. Capricornis), Darubini (Microscopium), Kuruki (Grus), Najari (Sculptor) na Ndoo (pia Dalu au lat. Aquarius).
Hutu Junubi (Piscis Austrinus) ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema الحوت الجنوبي al-ḥuut al-januubiy kwa maana ya “samaki ya kusini” . Waarabu walitafsiri hapa jina la Ptolemaio aliyetaja nyota hizi vile kwa jina la Νότιος Ιχθύς notios ikhthis katika orodha yake ya Almagesti; jina hili lilitafsiriwa pia kwa السمكة الجنوبية as-samaka(t) al-januubiya kwa kuitofautisha na Hutu au Samaki kwenye angakaskazi.
Piscis Austrinus - Hutu Junubi ni kati ya makundinyota 48 yaliyotajwa tayari na Klaudio Ptolemaio katika kitabu cha Almagesti wakati wa karne ya 2 BK. Iko pia katika orodha ya makundinyota 88 ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia kwa jina la Piscis Austrinus. Kifupi chake rasmi kufuatana na UKIA ni 'PsA'.
Kuna nyota moja tu ambayo ni angavu hii ni Alfa Piscis Austrini au Kinywa cha Hutu (en:Fomalhaut) . Ina mwangaza unaoonekana wa mag 1.16 ikiwa umbali wa miakanuru 25 na Dunia.
Jina la (Bayer) | Namba ya Flamsteed | Jina (UKIA) | Mwangaza unaoonekana | Umbali (miakanuru) | Aina ya spektra |
---|---|---|---|---|---|
α PsA | Fomalhaut (Kinywa cha Hutu) | 1,16m | 25,13 | A3 V | |
δ PsA | 4,2m | 170 | G8 III | ||
ε PsA | 4,2m | 744 | B8 V | ||
β PsA | 4,3m | 148 | A1 V | ||
γ PsA | 4,4m | ||||
η PsA | 5,4m | ||||
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Hutu Junubi (kundinyota), which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.