Hospitali ya Kilutheri ya Bulongwa inapatikana mkoa wa Njombe na inamilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ya Kusini Kati.
Hospitali hii ilifunguliwa mwaka 1968. Hospitali ya kilutheri ya Bulongwa ni hospitali ya rufaa yenye vitanda 120. Inapata misaada kutoka serikalini kupitia wizara ya afya kwa ajili ya wafanyakazi 27 na vitanda 90 tu. Hospitali hii inahudumia watu wapatao 60,000. Kuna wodi tano katika hospitali hii ya Bulongwa ambazo ni wodi ya wazazi, wodi ya wanawake, wodi ya wanaume, wodi ya watoto na wodi ya urekebishaji.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Hospitali ya Bulongwa, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.