Hifadhi Ya Taifa Ya Gombe

Hifadhi ya Taifa ya Gombe inapatikana kwenye mto Gombe, magharibi mwa Mkoa wa Kigoma, Tanzania.

Hifadhi Ya Taifa Ya Gombe
Sokwe wa hifadhi ya Gombe.
Hifadhi Ya Taifa Ya Gombe
Sokwe anayekula.
Hifadhi Ya Taifa Ya Gombe
Sokwe katika Hifadhi ya Gombe.

Ni hifadhi ndogo kuliko zote nchini ikiwa na kilometa za mraba 52 tu, lakini ina umaarufu mkubwa unaotokana na kivutio chake kikubwa ambacho ni sokwe.

Iko umbali wa kilometa 16 kaskazini kwa mji wa Kigoma, ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Kigoma.

Hifadhi hii ulianzishwa mwaka wa 1968, na ni ukanda mwembamba wa msitu wa mlimani unaokatizwa na miteremko mikali inayoingia katika mwambao wa mashariki wa Ziwa Tanganyika. Eneo hilo linajulikana na mabonde ya mwinuko, na mimea ya misitu inayotoka kati ya majani hadi mianzi ya milima hadi msitu wa mvua ya kitropiki.

Gombe ni miongoni mwa makazi machache yaliyosalia ya sokwe duniani. Hifadhi hii ilipata hasa umaarufu baada ya mtafiti wa tabia ya sokwe duniani, Jane Goodall kufanya utafiti juu ya maisha na tabia za sokwe wa Gombe kwa miaka 40 na kuandika vitabu kadhaa kuhusu viumbe hao. Jamii ya sokwe ya Kasakela, iliyo katika vitabu na hati kadhaa, huishi katika hifadhi hiyo.

Wanyama wengine wanaopatikana katika hifadhi hii ni pamoja na kima wenye mikia myekundu na kima wa bluu.

Wanyama wa jamii ya paka, kama chui na simba hawapo katika hifadhi hii na hivyo kuifanya kuwa salama kwa safari za miguu.

Wakati mzuri wa kutembelea hifadhi hii ni wakati wa kiangazi, Julai-Oktoba kwa sababu sokwe hawapendi kutembea nyakati za mvua. Chombo cha usafiri kitumikacho kwenda hifadhi ya Gombe ni mashua.

Tazama pia

Marejeo

Majarida ya hifadhi za Taifa Tanzania

Viungo vya nje

Hifadhi Ya Taifa Ya Gombe 
Wiki Commons ina media kuhusu:
Hifadhi Ya Taifa Ya Gombe  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kigoma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya Taifa ya Gombe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.

Tags:

MagharibiMkoa wa KigomaMto Gombe (Kigoma)Tanzania

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Bikira MariaMuundo wa inshaNabii IsayaHistoria ya UrusiMapenziWanyamweziUfufuko wa YesuNelson MandelaImaniKamusiMfalme SauliWakereweShahawaDiniSudanHoma ya mafuaIsraelAlama ya barabaraniTabiaTarakimuNyangumiMwongoChakulaKiingerezaWazaramoAli KibaMkalatusiJomo KenyattaMwanzoUtawala wa Kijiji - TanzaniaMuhammadKibena (Tanzania)AkiliSamliMMimba kuharibika2023Historia ya TanzaniaMisimu (lugha)SiasaFananiBabeliBangiBiasharaNyumbaHukumuLinuxAishi ManulaJamhuri ya Watu wa ZanzibarKamusi ya Kiswahili sanifuMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaNabii EzekieliOrodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifaNomino za wingiNuruAntibiotikiNduliUbatizoMtandao wa kijamiiWanyama wa nyumbaniMkoa wa RukwaMkoa wa TangaJeshi la Ulinzi la Wananchi wa TanzaniaKiambishiMethaliMorokoMkoa wa DodomaBibliaJoash OnyangoAteriMkoa wa GeitaSentimitaOrodha ya viongozi🡆 More