Ghuba Ya Aden

Guba ya Aden ni mkono pana wa Bahari Hindi kati ya Somalia upande wa kusini na Rasi ya Uarabuni upande wa kaskazini.

Inaanza kwenye sehemu ya Bahari Hindi iitwayo pia Bahari Arabu na kuelekea kwa mlango wa bahari wa Bab el Mandeb unaoiunganisha na Bahari ya Shamu.

Ghuba Ya Aden
Mahali pa Ghuba ya Aden


Eneo, visiwa, nchi na miji ya pwani

Ghuba hii ina urefu wa kilomita 1,000 na upana wake ni kati ya 150 km hadi 440 km. Kimo cha maji hufikia urefu wa mita 3,748. Imepakana na nchi za Yemen, Somalia (au Somaliland) na Jibuti.

Mabandari muhimu zaidi ni Aden nchini Yemen, Berbera nchini Somalia na mji wa Jibuti nchini Jibuti.

Kuna funguvisiwa viwili:

  • Sokotra ambayo ni sehemu ya Yemen
  • Visiwa vya Zeila mbele ya pwani la Somalia

Jiolojia

Kijiolojia ghuba ya Aden ni sehemu ya kaskazini ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki linaloendelea hapa chini ya uso wa bahari.

Bahari ya maharamia

Siku hizi ghuba hii ni kati ya njia za bahari hatari kwa usafiri kwa meli kwa sababu ya maharamia wenye vituo vya hasa Somalia lakini pia Yemen. Manowari za kimataifa zinajaribu kulinda eneo hili.

Tags:

Bab el MandebBahari ArabuBahari HindiBahari ya ShamuMlango wa bahariRasi ya UarabuniSomalia

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

TungoBinadamuMtume PetroJohn MagufuliWanyamweziHaikuSalaJihadiTiktokHifadhi ya mazingiraKalenda ya GregoriOrodha ya milima ya TanzaniaNetiboliKumaArudhiUislamuKima (mnyama)Kalenda ya mweziMkoa wa MbeyaOrodha ya miji ya MarekaniUvimbe wa koromeo usababishwao na streptokokiHarusiMotoKaswendeAnna MakindaNdege (mnyama)WaluguruInsha ya wasifuChatuFasihiNyanda za Juu za Kusini TanzaniaMuhammadTamathali za semiDhima ya fasihi katika maishaSoko la watumwaBaraOrodha ya maziwa ya TanzaniaMkoa wa TangaKuhaniMsibaTajikistanUbuntuJuxReal BetisOrodha ya watu maarufu wa TanzaniaLatitudoKylian MbappéLigi Kuu Uingereza (EPL)AganoOrodha ya shule nchini TanzaniaMohammed Gulam DewjiOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaNguzo tano za UislamuMsitu wa AmazonMazungumzoNchiKilwa KivinjeUjamaaSikioUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaOrodha ya Marais wa BurundiSiku tatu kuu za PasakaClatous ChamaNdiziOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaBiasharaMadinaAustraliaNgome ya YesuMsalaba wa YesuHistoria ya KanisaMkoa wa Morogoro🡆 More